Suluhu ya pekee hapa huwa ni kujamba ili kupunguza gesi hiyo tumboni
Sasa Wanayansi katika chuo kikuu cha
Exeter, nchini Uingereza, wanasema kuwa wamegundua harufu mbaya kama
vile ya kujamba japo inachukiza kwa pua, ina manufaa makubwa kwa afya ya
binadamu.
Wanasayansi hao wanasema kuwa harufu hiyo mbaya inaweza kuwa kinga dhidi ya magonjwa ya moyo na akili na hata Saratani.
Gesi au harufu mbaya ambayo hutokana na chakula kinachosagwa tumboni mwako inaweza kulinda baadhi ya viungo vya mwili wako.
Utafiti huo uliochapishwa katika mtandao wa chuo
kikuu cha Exter uligundua kuwa gesi hiyo inayojulikana kama Hydrogen
Sulfide ambayo pia hupatikana katika Mayai yaliyooza, inaweza kuwa
muhimu katika kutibu baadhi ya magonjwa.
"Ingawa gesi ya hydrogen sulfide inajulikana
kuwa na harufu mbaya na hupatikana katika Mayai yaliyooza pamoja na
harufu ya mtu kujamba, hutengezwa mwilini na inawezekana kuwa tiba kwa
magonjwa fulani,'' anasema Daktari Mark Wood,Profesa wa chuo hicho cha
Exeter.
Gesi hiyo ina athari mbaya ikiwa katika viwango vikubwa , kwa mujibu wa utafiti huo.
Watafiti wanasema licha ya harufu hiyo mbaya ya
kujamba kuchukiza, ina uwezo mkubwa wa kupunguza uwezekenano wa mtu
kupatwa na magonjwa kama vile, Saratani,Kiharusi, mshtuko wa Moyo na
kuumwa na mifupa
Chanzo: BBC
Chanzo: BBC

Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment