SERIKALI YAPOKEA MABEHEWA 25 YENYE THAMANI YA SH.BILIONI 4.3 KUTOKA INDIA
Get link
Facebook
X
Pinterest
Email
Other Apps
Waziri
wa Uchukuzi Dk.Harrison Mwakyembe (kulia), akiangalia moja ya mabehewa
kati ya mabehewa 25 mapya ya kubebea kokoto yenye thamani ya sh.bilioni
4.3 aliyoyapokea kutoka Kampuni ya M/S Hindusthan Engineering and
Industriles Limited ya India Dar es Salaam jana, kwa ajili ya Kampuni ya
Reli Tanzania (TRL). Wa pili kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TRL, Mhandisi
Kipalo Kisamfu. Waziri
wa Uchukuzi Dk.Harrison Mwakyembe (katikati), akifurahia jambo wakati
wa kupokea mabehewa hayo. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TRL, Mhandisi
Kipalo Kisamfu na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk.Shaaban Mwinjaka. Mkurugenzi Mkuu wa TRL, Mhandisi Kipalo Kisamfu (mwenye tai kushoto),akimuelekeza jambo Waziri Mwakyembe. Wafanyakazi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (PTA) na wa TRL wakishusha toka katika meli moja ya mabehewa hayo.
Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment