January Makamba aanza kuitikisa CCM......Ni kuhusu kauli yake ya Rais Kijana 2015....Yadaiwa anawza kusababisha mpasuko
KAULI
iliyotolewa hivi karibuni na Mbunge wa Bumbuli, mkoani Tanga ambaye pia
ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Bw. January
Makamba, akidai Tanzania kwa sasa inahitaji Rais kijana, imeanza kuibua
maswali kwa baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), mkoani
Shinyanga.
Katibu
Mwenezi wa CCM Wilaya ya Shinyanga mjini, Bw. Charles Shigino, alisema
kauli ya Bw. Makamba aliyoitoa akiwa nchini Uingereza inaweza
kusababisha mgawanyiko mkubwa ndani ya CCM kwa vile inaonesha ubaguzi wa
wazi kwa baadhi ya wanachama wake.
Akizungumza
na waandishi wa habari mjini Shinyanga jana, Bw. Shigino alisema yeye
binafsi anailaani kauli hiyo ambayo ameifananisha na siasa za ubaguzi
ndani ya chama ili kulibagua kundi moja la wanachama.
Alisema
CCM, imekuwa ikipinga suala la ubaguzi wa aina yoyote hivyo kauli ya
Bw. Makamba kutaka Rais ajaye mwaka 2015 awe kijana inaweza kusababisha
mpasuko kwani inapingana na Katiba ya CCM.
“Makamba
anapaswa kuelewa kuwa, ujana si kigezo cha kuwa na sifa za kugombea
nafasi ya urais, nafasi hii ni nyeti na mtu anayechaguliwa anapaswa kuwa
na busara, uwezo wa kuongoza nchi bila kuyumba.
“Wapo
wazee wenye sifa hizi kuliko vijana...kauli hii pia inapingana na
Katiba ya chama chetu labda paitishwe Mkutano Mkuu tuweze kufanya
mabadiliko ya Katiba vinginevyo hoja ya ndugu yetu haitakuwa na mashiko
kama wazee watajitokeza kuwania urais,” alisema.
Aliongeza kuwa; “Katiba
ya CCM Ibara ya 14 vifungu vidogo vya (1) hadi (3), vinafafanua wazi
juu ya haki za mwanachama ikiwemo ya kuomba kuchaguliwa kuwa kiongozi,
hapa haijataja wenye haki hiyo ni vijana tu, inawezekana Makamba,” alifafanua Shigino.
Alisema
ni vizuri Bw. Makamba akajifunza kutoka kwa wazee waasisi wa taifa hili
ambao waliwahi kuongoza nchi kwa ufanisi mkubwa badala ya kutoa kauli
zinazoashiria mianya ya ubaguzi ndani ya CCM hivyo kuhatarisha
mstakabali wa chama katika chaguzi zijazo.
“CCM
ni chama kikongwe nchini, ndani yake kuna akina mama, wazee na vijana
ambao wote wana haki sawa kwa mujibu wa katiba yetu, mimi sioni tatizo
la mgombea urais kwa tiketi ya CCM atokane na vijana au wazee, wote ni
sawa, mradi wawe na sifa, vigezo vinavyohitajika,” alisema.
Shigino
aliviomba vikao mbalimbali vya uteuzi ndani ya CCM, kuipuuza kauli ya
Bw. Makamba na wajumbe wake wasiwe tayari kuongozwa na matakwa ya watu,
bali wazingatie katiba na kanuni za chama katika uteuzi wao na muhimu
kuangalia mtu gani mwenye uwezo wa kuivusha CCM 2015 bila kujali ni mzee
au kijana.

Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment