Utafiti: Wanawake wengi wanafanya mapenzi kinyume cha maumbile huko Zanzibar
IMEELEZWA asilimia 25 ya wanawake wanafanya mapenzi kinyume cha
maumbile ama na waume zao au na wanaume wengine kama njia ya kukimbia
kupata ujauzito na mambo mengine.Takwimu hizo zimetolewa na Katibu wa
Jumuiya ya Maimamu Zanzibar kutoka wilaya ya magharibi, Sheikh Nassor
Hamad Omar, wakati akiwasilisha ripoti ya awali ya utafiti wa kamati ya
kupambana na vitendo vya liwati katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kusini
Unguja Tunguu, kwenye kongamano la vijana kuhusu udhalilishaji wa
kijinsia na mimba za mapema.Alisema takwimu hizo zimekusanywa kutokana
na utafiti uliofanywa na Jumuiya ya Maimamu (JUMAZA) katika maeneo
mbali mbali ya Zanzibar.Alisema sababu ya kufanya hivyo, ama wanawake
hao wanaogopa kupata ujauzito hasa wale ambao bado hawajaolewa lakini
wako kwenye mahusiano na hata wale walioko kwenye ndoa.Aidha alisema
utafiti huo umegundua watoto wengi wenye umri wa kuanzia miaka tisa
hadi 20, wanaingizwa katika vitendo viovu ikiwemo liwati na
usagaji.Alizitaja sababu kubwa zinazopelekea kuenea kwa uovu huo kuwa ni
pamoja
na tamaa, matumizi mabaya ya utandawazi, imani za kishirikina kwa
kupiga ngoma kama vile vibuki, kupenda kuiga tabia mbaya na watalii
wakorofi.Alisema kutokana na tatizo hilo, kamati yake imefanya utafiti
wa tatizo hilo na kutoa elimu kwa taasisi mbalimbali ambapo nyengine
zimekubali kushirikiana nao bega kwa bega ili kuondoa tatizo
hilo.Alisema Jumuiya imeandaa kitabu ambacho kimeandikwa kwa kuzingatia
zaidi misingi ya dini mbili za Kiislamu na Ukiristo.Aidha, alisema
wamefanikiwa kuvitembelea vyuo vya Quran na taasisi nyengine na
kukutana na walimu, wanafunzi, wazazi na walezi ili kufikisha ujumbe na
taarifa za utafiti huo.Akizungumza kwa huzuni kubwa Shekhe huyo alisema
inasikitisha kuona vijana wa kizanzibari wanafanya liwati huku wengine
wakishangiria na kuchukua picha.Nao vijana walioshiriki kongamano hilo,
wakichangia ripoti hiyo, wamekiri kuwa vitendo vya liwati vipo na ni
maarufu na vinafanywa kwa wingi hata maeneo ya vijijini. “Vyombo vya
habari vinapaswa kutumiwa kikamilifu kutambulisha na kutangaza uchafu
huu unaotia doa jamii ya Kizanzibari na taifa letu” alisikika mmoja wa
vijana hao akizungumza kwa masikitiko.Washiriki hao walisema kuwa
sheria zilizopo sasa zinatoa mwanya kwa wahusika kutotiwa hatiani na
kutoa nafasi ya kuendelea kufanya makosa.Walisema serikali kwa asilimia
kubwa inapaswa kuwajibika na ni lazima iweke mikakati imara ya kutunga
sheria ya kudhibiti suala hilo.Aidha, waliahidi kuvitumia vikundi vyao
kuelimisha juu ya mapambano hayo na kwamba watazitumia maskani zao
kulizungumzia tatizo hilokwa uwazi.Kongamano kama hilolinatarajiwa
kuendelea katika mkoa wa mjini magharibi.
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment