Kwa mujibu wa chanzo makini, mchongo huo ulifanyika kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram baada ya Shumileta anayesaka maisha nchini humo kuona picha ‘sex’ ya Lungi (iliyopo ukurasa wa nyuma), fasta akamtafutia mteja, raia wa Nigeria (jina kapuni).
Baada ya kumegewa mchapo huo, waandishi wetu waliingia mzigoni na kufanikiwa kunasa mawasiliano ya msanii wa filamu Bongo, Lungi Maulanga na Shumileta kupitia mtandao wa Instagram.
‘Charting’ hizo zilionesha ‘live’ kuwa Shumileta amemuomba Lungi amtafutie bwana huyo wa Kinaigeria, akafanikiwa kuwaunganisha na wakaanza kuchati kupitia Mtandao wa WhatsApp ambapo mwanaume huyo alimuahidi Lungi mambo makubwa ikiwa ni pamoja na kumtumia picha yake.
“Nyie mmepata wapi habari? Hiyo simu yangu ilipotea, nahisi mtakuwa mmeona mawasiliano yangu humo. Kwani Shumi kunitafutia bwana kuna tatizo gani? Bwana kaniona, kanipenda na mimi nimechati naye, kuhusu mambo ya kwenda Naigeria hiyo haiwahusu.”
Ili kuleta usawa wa habari, mapaparazi wetu walimtafuta Shumileta kwa njia ya simu, mambo yalikuwa hivi:
Mwandishi: Shumileta mambo vipi?
Shumileta: Safi, niambie.
Shumileta: Aliyekwambia nani? Mfuate muulize vizuri, mimi sizijui hizo habari.
Mwandishi: Mbona lakini kuna SMS zako zimefumwa kwenye simu ya Lungi ukimtafutia bwana?
Shumileta: Mfuate kamuulize mwenyewe.
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment
EmoticonClick to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.