| Wasanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Lady Jaydee (kushoto) akiimba sambamba na Professa Jay katika tamasha la burudani lililofanyika katika viwanja vya Leadars Club Kinondoni |
Mwanamuziki wa kundi la P square, Peter Okoye, akitoa burudani ya
aina yake kwa maelfu ya Mashabiki waliojitokeza katika viwanja vya
leaders club, Tamasha hilo lilidhaminiwa na Vodacom Tanzania burudani
hiyo ya karne ilitolewa kwa mashabiki wa muziki pale leaders club.
Mwanamuziki wa kundi la P square, Peter Okoye, akionesha uwezo wa
kulimudu gitaa tofauti na kuimba tu, wakati wa tamasha la burudani
lililofanyika katika viwanja vya leaders club, Wasanii hao mapacha
walikonga nyoyo za maelfu ya mashabiki waliojitokeza katika Tamasha hilo
lililodhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Mashabiki waliojitokeza katika tamsha la wasanii kutoka nchini Nigeria
Msanii Judith Wambura, Lady jay dee akiteta jambo na wasanii wa
musiki wa kundi la P-Square kabla hawajapanda jukwani na kutoa burudani
kali kwa maelfu ya mashabiki waliojitokeza katika Tamasha hilo
lililofanyika viwanja vya leaders club na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania
Dar es Salaam,
23 Nov 2013 . . Siku ya jumamosi mwezi huu pale leaders club ilikuwa
Usiku ya kihistoria kwa tasnia ya burudani nchini Tanzania baada ya
wasanii mapacha wa kundi la P Square, Peter na Paul Okoye kutoa burudani
ya aina yake ambayo haijapata kutokea kwa muda mrefu hapa nchini kwa
maelfu ya mashabiki wa burudani waliojitokeza katika viwanja vya leaders
club.
Wakiwa ni
wasanii wanaokonga nyoyo za mashabiki wa muzikini barani Afrika
walisindikizwa na wasanii kutoka hapa nchini ambapo jukwaa lilifunguliwa
na msanii Ben Pol ambaye alikonga nyoyo za mashabiki wa muziki kwa
kuimba kwa muziki wa bendi uliokuwa ukipigwa live na bendi ya machozi
bendi.
Huku hamu ya
mashabiki wa burudani ikianza kukolea kazi iliyofanywa vyema na
mwanadada Rady Jay dee iliwatoa jasho mashabiki waliofurika katika
viwanja hivyo, huku akiimba wimbo wa joto hasira uliopokelewa vyema na
mashabiki ulimshuhudia Profesar Jay akipanda jukwaani huku akichana
sehemu ya wimbo huo alioshirikishwa na mwanadada Anaconda.
Kazi ya burudani
kwa wasanii wa Tanzania ilifungwa vilivyo na msanii Jo Makini au mwamba
wa kaskazini alie limudu jukwaa na kuwapagawisha vilivyo mashabiki wa
muziki huku akisaidiwa vyema na msanii mwenzake Niki wa Pili ambao kwa
wasasa wanatamba na kibao chao cha tatizo ni bei ya mkaa kilicho
pokelewa vyema na mashabiki wao.
Ulifika wakati
ambao ulitarajiwa na maelfu wa mashabiki waliojitokea katika viwanja vya
leaders club ambapo wasanii Peter na paul okoye, walipopanda jukwaani
na kuanza kutoa burudani kwa mashabiki. Wasanii hao walianza kwa
kuwashukuru mashabiki waliojitokeza na kuishukuru kampuni ya Vodacom kwa
kufanisha ujio wao hapa nchi.
P Squre walitoa
burudani ya kipekee kwa muda wa masaa mawili mfurulizo bila ya kuchoka
na kila walipoweka kibao kingine ndipo moto wa mashabiki ulizidi kuwaka
na kukidhi vilivyo kiu ya mashabiki wa burudani.
Burudani ya
kipekee ilikuwa pale ambapo wasanii hao walianza kuonesha vipaji tofauti
walivyonavyo, huku Peter akionesha uwezo wa kupiga gitaa vilivyo
alijibiwa na kaka yake Paul akijibu mapigo kwa kupiga vilivyo ngoma huku
wakipokea shangwe kutoka kwa mashabiki wao.
Shukurani za
kipekee kwa kampuni ya Vodacom Tanzania iliyofanikisha ujio wa wasanii
hawa waliotoa burudani ya kipekee kwa Watanzania hakika itakuwa ni
historia ya aina yake kwa tasnia ya burudani na fundisho kwa wasanii wa
hapa nchini.
Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment