LULU AKANUSHA KUCHUMBIWA,ASEMA UKIWA MPANGO WA MUNGU ATACHUMBIWA NA ATAOLEWA ILA KWASASA YEYE BADO...
Muigizaji wa filamu nchini Elizabeth Michael
aka Lulu amekanusha
fununu zilizoandikwa kwenye gazeti la udaku liitwalo ‘Filamu’ kwamba
amechumbiwa na muda mchache ataolewa.
Akizunguza jana kwenye kipindi cha XXL cha
Clouds FM, muigizaji huyo
wa Foolish Age, alisema hajachumbiwa na mtu yeyote ila ni magazeti ya
udaku tu ndio yamekuwa yakiandika kile yanachojisikia.
“Mimi sijachumbiwa na hakuna mtu yeyote
aliyenichumbia na kama
itatokea siku nikachumbiwa kila mtu atajua, na ni mimi mwenyewe ndiye
nitakaesema,” alisema mrembo huyo.
“Lakini sasa sijajua wao wamepata hiyo habari
kutoka kwenye chanzo
gani, by the way kwaajili kumekuwa na habari kila kukicha kila mtu
anayejisikia kuandika anaandika ,anaamka anaandika, anaamka anandika.
"Kwa hiyo leo wameandika nimechumbiwa, kesho
wataandika nimeolewa, kwa hiyo
inategemea na mood ambayo wao waliamka nayo, kwamba ‘leo Lulu
tumchumbie, tumuozeshe, tumuachishe’, I don’t know.
“Kuchumbiwa, kuolewa,kuwa mke ni vitu ambavyo
tumeumbiwa binadamu,
vipo kama ukiwa mpango wa mwenyezi Mungu nitachumbiwa na nitaolewa.”
Lulu

Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment