MAWAZIRI
watatu wa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete wapo katika wakati mgumu
baada ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Nape
Nnauye, kutangaza rasmi kuwa atahakikisha wanachukuliwa hatua za
kuwajibishwa kutokana na kushindwa kutekeleza majukumu yao.
Wakati Nape akitaka mawaziri hao watimuliwe, Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulhaman Kinana, amesema kuwa mawaziri hao watawekwa kiti moto katika
kikao kijacho cha Kamati
Kuu (CC), kwa lengo la kueleza ni hatua gani wanachukua katika
kushughulikia matatizo ya Watanzania.
Kuu (CC), kwa lengo la kueleza ni hatua gani wanachukua katika
kushughulikia matatizo ya Watanzania.
Mawaziri hao ni Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhandisi
Christopher Chiza, Naibu wake, Adamu Malima na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa ambaye ametajwa kuwa sehemu ya matatizo katika kila wizara anayopewa kuiongoza.
Christopher Chiza, Naibu wake, Adamu Malima na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa ambaye ametajwa kuwa sehemu ya matatizo katika kila wizara anayopewa kuiongoza.
Akizungumza
jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Wilaya ya Namtumbo
mkoani Ruvuma, Nape alisema hakuna sababu ya kukaa kimya wakati mawaziri
hao wameshindwa kazi, hivyo ni vema wakawajibishwa ili kukiokoa chama
chao.
Kuhusu
Chiza na Malima, Nape alisema mawaziri hao wameshindwa kutekeleza
wajibu wao kwani tangu walipochaguliwa kuongoza wizara hiyo hakuna hata
siku moja ambayo wamefika Ruvuma kushughulikia matatizo ya wakulima
wakiwamo wa korosho, tumbaku, mahindi na mpunga, ambapo katika mikoa
mbalimbali nchini imekuwa ikilalamikia sekta ya kilimo lakini wenyewe
wamekaa kimya bila kuchukua hatua zozote.
“Katibu
Mkuu leo ni bora nikazungumza haya ya mawaziri ambao wamepewa dhamana
ya kuwatumikia Watanzania. Nimeuliza hapa Ruvuma Waziri wa Kilimo na
naibu wake walishawahi kufika mara ngapi kushughulikia matatizo ya
wakulima. Jibu lake, hakuna hata siku moja wamefika.
“Hii
inaleta tabu, wakati wakulima wanahangaika na pembejeo za kilimo,
ukosefu wa soko na malipo ya fedha wanazodai serikalini mawaziri wenye
dhamana wapo mjini wanafunga tai na suti. Hawafikiri kuhusu matatizo ya
wakulima,” alisema.
Aliongeza
kuwa yupo tayari kupoteza nafasi yake lakini hawezi kuvumilia hali hiyo
ikaendelea na kutumia nafasi hiyo kumuoma Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana, ahakikishe wanachukuliwa hatua na ikiwezekana waitwe
CC wahojiwe.
Alisema
karibu Tanzania yote wakulima wamekuwa na matatizo mengi na wamekuwa
wakilalamikia wizara hiyo na yeye ni shahidi wa hayo yanayoendelea
kutokea na ili kukinusuru chama hicho mawaziri walioshindwa kazi
wawajibishwe.
Alisema
kuwa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika imepewa dhamana ya
kuwatumikia Watanzania asilimia 80, ambayo ni wakulima lakini waliopewa
jukumu hilo hawataki kufanya kazi zao.
“Wananchi
naomba mnilinde, lakini niseme ukweli. Niseme nisiseme…mawaziri ambao
tumewapeleka jikoni wameshindwa kupika chakula, tunasubiri sebuleni
lakini chakula hakiji. Wanatukwamisha, ni bora wakaondoka kama
wameshindwa kazi.
“Katibu
Mkuu mimi nikija, sipo tayari kuona CCM inakuwa chama cha upinzani
bungeni kwa sababu tu ya hawa wenzetu wachache ambao wanafanya makusudi
na uzembe katika kutekeleza wajibu wao,” alisema Nape.
Wakati
kwa Dk. Kawambwa mbali ya kushindwa kuongoza Wizara ya Elimu na Mafunzo
ya Ufundi naye anatakiwa kuchukuliwa hatua kutokana na mkataba
aliouingia na makandarasi wa ujenzi wa barabara ya kutoka Namtumbo hadi
Tunduru mkoani Ruvuma.
Nape
alisema anamshukuru Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, kwa kumfukuza
mkandarasi huyo aliyemtaja kwa jina la Progressive ambaye ameshindwa
kazi ya kujenga barabara hiyo.
Hata
hivyo, kumfukuza mkandarasi huyo pekee haitoshi, hivyo aliyehusika
kumpa mkataba anapaswa kuchukuliwa hatua kwani uchunguzi unaonesha kuwa
alishashindwa kazi na wakati anapewa mkataba huo Waziri husika alikuwa
Dk. Kawambwa.
“Dk.
Kawambwa amekuwa akitukwamisha CCM katika kutimiza wajibu wake. Hii
barabara ya Namtumbo hadi Tunduru kushindwa kukamilika imeleta aibu
kubwa na kututia fedheha. Hivyo lazima waliotoa mkataba wawajibishwe.
“Dk.
Kawambwa huyu huyu ameshindwa kushughulikia matatizo ya walimu nchini
na atambue kuwa tulimpa muda wa miezi sita na sisi tunahesabu,
ukimalizika hatutaacha kuchukua hatua.
“Chama kitatumia wabunge wake kumuwajibisha. Hatuwezi kukaa kimya.
Iwapo
ninaonekana kama kero kwa kupigania masilahi ya nchi na watu wake, nipo
tayari kuondoka na kwenda kujihusisha na kilimo. Maana mimi ndiye mpiga
debe wa chama, nitakwenda kueleza nini kwa umma kutokana na ahadi zetu
kukwama kwa sababu tu ya uzembe wa wachache ndani ya serikali?” alihoji.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa CCM, Kinana, alisema kuwa katika kikao
kijacho cha Kamati Kuu (CC), kitakachofanyika Desemba mwaka huu chama
kitamuandikia barua Rais Jakaya Kikwete ili mawaziri wake waje wajieleze
mbele ya kikao kwa nini wasifukuzwe kwa kushindwa kazi.
CREDIT: TANZANIA DAIMA

Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment