![]() |
Julius Nyaisanga a.k.a Anko J (katikati) akiwa katika picha ya pamoja
na Mkongwe Mwenzie,Aboubakar Liongo .
|
HABARI zilizotufikia kutoka mkoani Morogoro ni kwamba Mtangazaji Mkongwe nchini, Julius Nyaisangah 'Uncle J' ameaga dunia. Mpaka mauti yanamfika, Marehemu Nyaisangah alikuwa Mhariri Mtendaji wa Abood Media iliyopo mkoani Morogoro. Marehemu aliwahi pia kufanya kazi katika kituo cha Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD) na katika Kituo cha Redio One ambapo alikuwa Mkurugenzi. Mpaka sasa chanzo cha kifo chake bado hakijafahamika japo marehemu alikuwa akiugua kwa muda mrefu. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN! Taarifa zaidi zitawajia baadaye

Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment