Tunda Man atoa wimbo wa Qaswida kama zawadi ya Ramadhan.

Msanii wa kundi la Tip Top connection, Tunda Man leo ametoa zawadi ya wimbo wake wa Qaswida kwaajili ya mashabiki wake na ambao atawatumia kwa email ama Whatsapp.
561160_568978193128945_1425014148_n
Tunda Man amesema kuwa huu wimbo ni zawadi kwa wadau wake wanaofuatilia muziki wake na kutambua mchango wao.
“Nimetoa wimbo wa qaswida kwaajili ya mashabiki wangu, ni zawadi ya mwezi mtukufu kwahiyo nimeimba mwenyewe. Atakayeuhitaji nimeandika status Facebook ata comment kuandika Email au Whatsapp ili nimtumie.”

Comments