
Mwanamke mmoja mfaransa (52) amejikuta
mikononi mwa polisi
wa jiji la Paris katikati ya mwezi june, baada ya kukamatwa kwenye
chumba cha
mtihani akimfanyia mtihani wa Kiingereza mwanae mwenye umri wa miaka 19,
huku
akijiweka kisichana zaidi wasimshutukie.
Ripoti kutoka nchini humo zinasema mwanamke
huyo
aliyejulikana kwa jina la Caroline D aliingia kwenye chumba cha mtihani
akiwa
amevaa skin jeans na viatu aina ya Converse ili aonekane kama mwanae.
Lakini jicho makini la msimamizi wa mtihani
lilimnasa mama
huyo kwa kuwa msimamizi alikua tayari alishamuona mwanae wakati anafanya
mtihani wa Philosophy, kwa hiyo akamshtukia mama huyo kwa muonekano wake
na
sura yake ya kiutu uzima.
Msemaji wa Polisi wa Paris alisema mwanamke
huyo alikiri
makosa yake ya udanganyifu na kusema kuwa kiukweli yeye alikuwa anaweza
zaidi
Kiingereza zaidi ya mwanae.
Mwanamke huyo anakabiriwa na mashtaka ya
udanganyifu na
anaweza kulipa fine isiyopungua £7,000.
Lakini pia binti yake anaweza kupata msala wa
kuzuiwa
kufanya mtihani wowote wa kitaifa kwa muda wa miaka mitano.
LeoT
LeoT
Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment