0
Mtangazaji wa Channel Ten ambaye pia ni mwigizaji na mtayarishaji wa filamu, Bond Bin Suleiman na Elizabeth Michael aka Lulu wameiwakilisha vizuri Tanzania kwenye tamasha la filamu la kimataifa Zanzibar, ZIFF zilizofanyika ngome kongwe,Zanzibar.
BOND
Lulu amefanikiwa kuchukuwa tuzo ya mwigizaji bora wa kike kupitia fialmu Women of Principal akitumia jina la Linda na Bond amepata tuzo kupitia filamu yake ya “ Lover’s Island” ambayo imemfanya aweze kunyakua tuzo tatu zikiwa pamoja na mwigizaji bora wa kiume,mwongozaji bora na filamu hiyo kuchaguliwa kuwa filamu bora ya mwaka 2012/2013. Filamu hiyo ameigiza na wasanii wengine nyota akiwemo Richard, mshindi wa Big Brother Africa 2.
woman_of_principles
“Filamu yangu ya Lover’s Island imekuwa filamu Bora ya mwaka 2012/2013, nimekuwa mwigizaji bora na mwongozaji bora na Lulu amekuwa mwigizaji bora wa kike kupitia filamu ya Women of Principal. Kwahiyo tunawashukuru wale waliotuchagua na kuona ubora wa kazi zetu na tuna wahaidi Watanzania kufanya mambo makubwa zaidi katika fialmu.
377360_306335786046214_2085293898_n

Post a Comment

toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment

 
Top

SOMA HABARI KEM KEM KUPITIA BLOG YAKO PENDWA YA HISIA ZA MWANANCHI HAPA

X