Kufuatia
kuwa na safu ya ulinzi inayovuja kwa sasa, miamba ya soka nchini
Hispania na Dunia nzima ambayo inamiliki mchezaji bora wa FIFA mara nne
mfululizo, Lionel Andrew Jorge Messi, nawazungumzia wazee wa Katalunya,
FC Barcelona, wametuma ofa ya pauni milioni 30 kwa klabu ya Chelsea ili
kumsajili beki raia wa Brazil, David Luiz, lakini inasemekana miamba ya
darajani itapotezea dau hilo.
Barca
ambao beki yao inayumba sana kwa sasa wanajiandaa kumsajili mlinzi bora
wa kati ambaye atadumu kwa muda mrefu na kumrithi mkongwe na nahodha
wao CarlesPuyol ambaye soka linafikia ukiongoni kutokana na kuwa na mvua
za kutosha.
Vyanzo
vya habari vinaeleza kuwa Luiz kubaki Chelsea ni asilimia hamsini kwa
hamsini, lakini alikuwa mhimili mkubwa katika kikosi hicho tangu ajiunge
nacho mwaka 2011 akitokea Benfica.
Dau
lake lipo juu: David Luiz ni miongoni mwa mabeki wazuri ligi kuu soka
nchini England
Luiz
naweza kucheza na Gerard Pique pamoja na Mbrazil mwenzake, Neymar
katika dimba la Camp Nou
Licha
ya kucheza na Pique au Puyol moja ya mabeki imara, Luiz atacheza na
Mbrazili mwingine Dani Alves
Msimu
uliopita, Barca walihangaika sana baada ya Puyol kukaa nje ya uwanja,
na kulazimika kuwachezesha viongo Javier Mascherano au Alex Song kucheza
nafasi yake, na ndio maana wanahitaji beki mzuri wa kati.
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment