Watu 92 wamefikishwa katika Mahakama ya Mkoa wa Mtwara na kusomewa mashitaka mbalimbali, ikiwamo kufanya fujo, kuvunja nyumba, kuiba, kujeruhi na kuhujumu uchumi katika vurugu zilizotekea mjini Mtwara, Mei 22, mwaka huu.
Watu hao walifikishwa mahakamani hapo
mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Mussa Esanju.
Waendesha
Mashitaka wa Serikali, Justine Sanga, na Renatus Mkude, walidai kuwa
washitakiwa hao walitenda makosa hayo katika tarehe hiyo.
Watuhumiwa kwa pamoja walikana mashitaka
hayo na kurudishwa rumande.
Uamuzi
huo unatokana na wengi wa washtakiwa kukabiliwa na tuhuma za kuhujumu
uchumi, kosa ambalo mahakama hiyo haina uwezo wa kuwaachia kwa dhamana.
Hakimu Esanju aliiahirisha kesi hiyo
hadi Juni 10, mwaka huu, kwa ajili ya kutajwa.
HABARI IMEANDIKWA KWA KIREFU KATIKA
GAZETI LA NIPASHE

Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment