Mlinzi wa baa ya Darajani Stop Over iliyo kando kando ya barabara kuu ya Morogoro Dar es salaam jirani na daraja la Mzambarauni Bw Mika Athumani amechinjwa na majambazi usiku wa kuamkia leo.
Habari zilizopatikana eneo la tukio zilidai kwamba majambazi hayo yalivamia baa hiyo iliyojitenga usiku wa manane na kumvamia mlinzi huyo na kumchinka kama kuku na baadae kuvunja baa hiyo na kuimba vitu mbali mbali.
Mwili wa marehemu ukiwa ndani ya gari, la polisi kufuatia mwili huo kutenganiswa vibande viwili..
Sehemu aliyochinjiwa mlinzi huyo
aliyefahamika kwa jina Mika Athumani.
Akihojiwa na mwandishi wetu,
mmiliki wa baa hiyo Bw Salvatory
Mushi alidai kwamba majambazi hao walimvamia mlinzi wake na kumchinja na
baadae walivunja Counter ya baa hiyo pamoja na duka ililipojirani na
baa hiyo na kuiba vitu mbali mbali.
Alipoulizwa kwamba kuna taarifa zinadai kwamba mlinzi huyo alikutwa akiwa amelala Bw Mushi alisema" inawezekana lakini hakuna mtu mwenye uhakika na jambo hilo kwani sote hatukuwepo,wakti tukio hilo linatokea"

Alipoulizwa kwamba kuna taarifa zinadai kwamba mlinzi huyo alikutwa akiwa amelala Bw Mushi alisema" inawezekana lakini hakuna mtu mwenye uhakika na jambo hilo kwani sote hatukuwepo,wakti tukio hilo linatokea"
Mwananachi akishuhudia damu ya
mlinzi huyo kwa hudhuni
Baskeli ya Mlizni huyo ikiwa
imetapakaa damu ambapo inadaiwa mlinzi huyo alikuwa amelala kwenye eneo
hilo
Redio ambayo majambazi hayo
waliiangusha nje ya baa hiyo
Majaira ya saa 12 asubuhi ya leo
wananchi walishuhudia maduka mawili
ya baa hiyo yakiwa wazi huku mwili wa mlizni huyo umekutwa upande wa
baa ukiwa umechinjwa na kutenganishwa kichwa na mwili
Umati wa watu ukishuhudia tukio
hilo muda mfupi uliopita
Gali la polisi likiondoka eneo la
tukio na mwili wa marehemu
Wananchi nao waliondoka eneo hilo
la tukio
Mmiliki wa baa hiyo Bw Salvatory
Mushi akihojiwa na waandishi wa habari eneo la tukio
Majirani wa eneo hilo wakihojiwa na waandishi wa habari
Baadhi ya watu waliokuwepo eneo
hilo la tukio walidai kwamba
mlinzi huyo alikuwa amelala hivyo majambazi hayo yalimvamia na kumpora
siraha zake na kishi kumchinja shingoni..
Mwandishi wetu alishuhudia mtoto
wa marehemu pamoja na
mjukuu wa marehemu wakiangua vilio eneo la tuko baada ya kuuona mwili wa
mazazi wao aliyeuwawa kikatili baadae wote wawili walipanda gari la
polisi na kuondoka nao.

Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment