MJUE DIWANI WA CHADEMA ANAYEFANYA VIZURI RUNZEWE NI YUSUFU FUNGAMEZA MSOME HAPA....

MH YUSUFU FUNGAMEZA

Ukilitaja  Jina la YUSUFU FUNGAMEZA katika mji wa Runzewe ni kama umemtaja Raisi kwa jinsi wanavyomkubali.Huyu ni muheshimiwa diwani kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA).Kama jina la chama chake linavyosomeka chama cha maendeleo, kweli kaleta maendeleo makubwa ndani ya mji wa Runzewe na amani imetawala sana ndani ya mji huo.

  Kwanza kabisa ukifika Runzewe utakuta kuna stendi nzuri sana pale japo sio kubwa sana lakini kwa mzingira ya mji huo inatosha sana.Hapa awali mji wa Runzewe hakuwa na stendi kabisa watu walikuwa wanasubilia magali barabarani lakini kwa sasa ipo stendi .

   Pili mitaani kwa sasa kuna barabara. tofauti na hapo awali kulikuwa hakuna barabara  lakini kwa sasa safi kabisa. Na kwa tathmini mradi wa barabara umeghalimu sh milion 28.Na kwa mujibu wa muheshiwa ni  kwamba amerekebisho ya barabara hizo ili baadaye mladi wa umeme ukifika wasipate tabu sana.

   Pia amepigania sana mladi wa maji kwa sasa kuna mabomba ya maji yapo mtaani japo sio mengi lakini yanasaidia kwani maji unayapata kwa bei raisi sana tofauti na hapo awali watu walikuwa wanyapata kwa bei ya juu sana tena kwa tabu sana.na mradi huo umegalimu sh m 180.

  Kwa upande mwingine muheshimawa diwani uyo kapanuwa mji kiasi chake kwani kaweka soko pembeni mji kidogo eneo linaitwa IBAMBA ilo ni Gulio ambalo wakulima uja kwa ajili ya kuuza na kununa bidhaa na mazao tofauti. Na Gulio hilo ni la siku 3 yaani Jumamosi, Jumanne na Alhamisi mnakaribishwa sana wote.

  Ni mengi sana ameyafanya muheshimiwa huyu mengineyo ni kama vile uduma ya upasuaji pale hospitali na kaleta gali la wagonjwa yaani AMBULENCE kwa sababu ya kusaidia wangonjwa wanaoshindwa kutibiwa hapo wanapelekwa Wlayani ambapo ni Bukombe.Bila kusahau kuna machinjio ya kisasa ambayo yataghalimu sh m 60. Hayo yatakuwa ni machinjio ya kisasa ambayo yatakuwa na kila kitu muhimu kinachotakiwa kwenye machinjio.

  Bila kusahau ameapigania na kuanzisha shule mpya ya msingi bila ya michango ya wananchi na hii imetokana na rasimari za mji huo wa Runzewe . Shule hiyo ipo maeneo ya Kanembwa na sasa imefikia kwenye Lenta ina vyumba vya madarasa vitano na ofisi moja ya walimu. Matajio yake mwaka huu mwezi wa saba watoto waanze kusoma hapo.

   Kwa upande wetu SHEBBY D BLOG tunampongeza sana kiongozi huyo wa CHADEMA kwa kuwajibika ipasavyo najua  bado mji haujakaa sawa sana lakini kwa haya tunampa ongera yake kwani inaonyesha akitawala tena miaka mitano ijayo mji utkuwa uko juu sana.

Comments

Post a Comment

toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment