| Kwa ujumla mtoto Joshua hata kutembea hawezi kwani simama yake ni ya kutetemeka migu tu |
| Hizi ni nguo za joshua na kaka yake nguo hizi hazifuliwi bali zikirowa na mkojo huwanikwa tu juani na kisha kuvaliwa tena |
| Mtoto Joshua akiwa ana tushangaa maana anaona amevamiwa kwakweli inasikitisha sana |
| Hapa ndiyo mtoto joshua huwa anacheza wakati wa mchana |
| Mlango ulio wazi ndimo mtoto Joshua hufungiwa humo |
| Hiki ndicho chumba mtoto Joshua hufungiwa kama picha unavyoiona kona hiyo ndiyo mtoto huyo hujibanza |
| Kushoto ni kaka wa Joshua yeye amesema huwa anashinda nyumba za jirani kucheza wakati mdogo wake amefungiwa ndani |
| Angalia picha hii kwa makini jinsi mtoto Joshua anavyomwangalia mama yake mlezi yaani mama wa kambo. |
| Sekera Watsoni (40) amembeba mtoto Joshua kuonyesha anampenda na kuwa anamhudumia vizuri mtoto huyo. |
| Huyu mama pamoja na mumewe ndiyo wanaomtesa mtoto Joshua. |
| Hawa kaka zake Joshua wakituonyesha sehemu wanayolala pamoja na joshua wakati mama huyo yeye amesema yeye huwa analala na joshua chumbani kwake |
| Baadhi ya majirani wakisimulia mkasa huo. |
| Amini usiamini mtoto Joshua baada ya kuona mkeka mzuri alijilaza kwa furaha kwani amezoea kulala sakafuni. |
| Mama mlezi wa Joshua akijiandaa kumpeleka joshua kituo cha afya akapate matibabu baada ya kuamriwa kufanya hivyo. |
|
Habiba
Ibrahimu amesema kuwa tukio la kufungiwa ndani mtoto ni la aibu kubwa
hivyo
halipaswi kufumbiwa macho na jamii husika hivyo ametaka hatua za haraka
zichukuliwe ili kuokoa maisha ya mtoto huyo
Katika hali isiyokuwa ya
kawaida mtoto mwenye umri wa zaidi ya miaka miwili amefungiwa ndani na
wazazi
wake kwa kipindi cha miaka miwili sasa bila kutoka nje pamoja na kukosa
matunzo
muhimu hali ambayo imepelekea mtoto huyo kudhoofu kiafya.
Tukio hilo limetokea leo
jijini mbeya katika mtaa wa Ikuti kata ya Iyunga ambapo majirani wa
karibu na
mtoto huyo pamoja na baadhi ya viongozi wa mtaa huo kufika nyumbani
anapoishi
mtoto huyo kwa lengo la kufahamu maendeleo yake .
Mtoto huyo amefahamika
kwa jina la Joshua Joseph umri unao kadiriwa kuwa ni kati ya miaka
miwili au
mitatu ambaye alikutwa nyumbani hapo akiwa pekee yake huku wazazi wake
wakiwa
wameondoka kuelekea kwenye shughuli zao.
Akizungumzia tukio hilo
Kaimu barozi wa mtaa huo wa Ikuti Ndugu Aloni Mboya amesema kuwa hali
hiyo
imenza kujitokeza kwa kipindi cha miaka mitatu sasa hali ambayo
imepelekea mtoto
huyo kukumbwa na maradhi ya utapiamlo.
Amesema katika kipindi
cha mwaka 2011 mwezi wa tatu alipokea taarifa kuhusiana na suala hilo
ambapo
baba wa mtoto huyo ndugu Joseph Simoni aliitwa katika ofisi za mtaa kwa
lengo la
kumhoji juu ya malezi ya mtoto huyo.
Aidha baada ya kuhojiwa
alikiri kosa ambapo alipewa onyo na viongozi wa mtaa ambao walimtaka
kuhakikisha
anamtunza vema mtoto huyo kwa kumpatia chakula bora pamoja na huduma
nyingine.
Mara baada ya mtu huyo
kupewa kalipio na viongozi wa mtaa hali hiyo iliendelea tena ambapo wao
kama
viongozi wa shina pamoja na wananchi walimuita yeye pamoja na mke wake
aitwaye
Sekera Watsoni (40) kuhama mtaani hapo kwa kwa kipindi cha miezi sita
ambapo
walikaidi agizo hilo.
Amesema mara baada ya
watu hao kugoma waliamua kuwaacha na kuwaondoa katika umoja wa ubarozi
wao na
kuto watambua tena kama wananchi wa eneo hilo kutokana na vitendo vyao
vya
kikatili dhidi ya mtoto huyo.
Kwa upande wao Maafisa
maaendeleo ya jamii kata ya Igawilo na Iyunga ambao ndio waliofika
katika eneo
hilo wamesema kuwa matukio kama hayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara
ndani
ya jamii hasa kwa vitendo vya kunyanyaswa kwa watoto
wanawake.
Mmoja wa Maafisa hao
Ndugu Habiba Ibrahimu amesema kuwa tukio la kufungiwa ndani mtoto ni la
aibu
kubwa hivyo halipaswi kufumbiwa macho na jamii husika hivyo ametaka
hatua za
haraka zichukuliwe ili kuokoa maisha ya mtoto huyo.
Amesema hali ya kiafya ya
mtoto si ya kulizisha kutokana na kusumbuliwanna maradhi mbalimbali
yanayotokana
na kukosekana kwa lishe bora pamoja na huduma nyingine.
Amesema anawashukuru
majirani pamoja na viongozi wengine wa serikali ya mtaa ambao wamekuwa
karibu na
mtoto huyo kwa kipindi chote cha miaka miwili licha ya kutokuwepo kwa
ushirikiano toka kwa wazazi wa mtoto ambaye kwa sasa amefikishwa katika
kituo
cha afya Inyala Kata ya Iyunga jijini hapa.
Awali inaelezwa kuwa baba
na mama wa mtoto huyo wamekwisha tengana kwa kipindi kirefu sasa
kutokana na
kutokuwepo kwa maelewano ndani ya nyumba hiyo hali ambayo ilimfanya baba
huyo
kuoa mwanamke mwingine ambaye ndiye anaye ishi na mtoto kwa sasa kama
mama wa
kambo.
Amesema kutoka na kuwepo
kwa mgawanyiko huo ndani ya familia baba pamoja na mama huyo ambaye ni
mke wa
pili walichukua jukumu la kuishi na watoto wote walio achwa na mwanamke
wa
kwanza ambapo kwa asilimia kubwa ndiko kuliko sabababisha kuwepo kwa
hali hiyo
ya manyanyaso ya mtoto.
Hata wakati wa tukio hilo
la kumtoa mtoto huyo ndani baba mzazi wa mtoto hakuwepo katika maeneo
hayo ya
nyumbani ambapo maafisa ustawi wa jamii pamoja na majirani waliamua
kuchukua
jukumu la kumpeleka mtoto huyo katika kituo cha afya Inyala kilichopo
Kata ya
Iyunga kwa lengo la kumfanyia uchunguzi na kutambua nini kinacho msumbu
|
Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment