Msanii Linah
Barnaba
KUELEKEA shoo maalumu ya Miaka 13, ya
mwanamuziki nguli wa bongo fleva nchini na kiongozi wa bendi yenye
msisimko mkubwa ya ‘Machozi Band’, Judith Wambura ‘Lady Jay Dee’ au
Jide’ huenda kwa upande wa wasanii wa Nyumba ya Vipaji ya THT, Linah
Sanga na Barnaba mwaka huu ukawa mchungu kwao kufuatia kuwepo taarifa
za kutimuliwa na uongozi wa juu.
Kwa mujibu wa vyanzo kutoka kwa mtu
wa karibu wa Linah kilieleza kuwa mpaka sasa msanii huyo hana raha na
wala hajui ataanza vipi katika harakati zake za kimuziki hasa kufuatia
hivi karibuni kukacha shoo ya nguli Lady Jay Dee kwa shinikizo kutoka
kwa wakubwa zake.
Hata hivyo, Linah inadaiwa uongozi wa
juu umekaa kikao na hatua iliyofuatia kwenye kikao hicho ni kuwaondoa
kabisa kwani huenda wakatia doa wasanii wenzao ndani ya kundi hilo.
“Juzi Lina,haikuwa kawaida yake maana
hata alipopigiwa simu na ** kwa ajili ya hatua zingine alionekana kuw
na hofu, na wala hakutaka kusikia ushauri wangu ambao nilikuwa
nikimhusia kuwa aachane na mawazo hayo kwani jambo analoliwaza huenda
likaisha na hata maamuzi yatakayotoka yatakuwa ni kawaida” kilieleza
chanzo kutoka kwa mtu wakaribu wa Lina, amabaye hata hivyo alisema kuwa
huenda ukweli wa jambo ukawa hadharani.
Hata hivyo taarifa za ndani za
uongozi wa THT zilibainisha kuwa mpango wao wa kuwashughulikia wasanii
hao upo pale pale na taratibu zinafuata ili zisilete madhara kwa wasanii
waliopo ndani ya THT na watu wa karibu wanaoiunga THT.
“Wewe nani kakwambia kama
tumewaadhibu Lina na Barnaba?, ndio kwanza tunakusikia wewe hizo
taarifa, sisi tunafanya mambo yetu wao waache wafanye yao tukiwa nao
sie na tunao uwezo wa kuwatimua ilikulinda hadhi ya THT” Kilieleza
chanzo hicho ambacho hata hivyo kutokana na usalama wa jina lake
tumelihifadhi. Ambapo namba yake inaishia na**08.
Aidha, katika ‘ku-balance’ huondo
kamili wa habari hizi wasanii hao wote walipotafutwa kwenye simu zao za
mkononi lakini hawakuweza kuwa hewani kwa muda mrefu.. na hata
alipopigiwa mtu wao huyo wa karibu naye alizima simu.
Katika kile kinachoeleza kupamba moto
shoo hiyo, na kujaa kwa taarifa mbalimbali juu ya wasanii watakaopamba
shoo ya miaka 13, Mei 31 ndani ya Nyumbani Lounge, Tayari tiketi
zimeanza kuuzwa maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Saalam.
Shoo hiyo ya kijanja Nyumbani Lounge,
patakuwa hapatoshi pale wadau wa burudani na wastaarabu wote
watakapojumuika kwa pamoja ku-shoo love kwa Lady Jay Dee na Machozi
Band, huku listi ya mastaa mbalimbali wanatarajia kuudhuria sambamba na
‘surprise’ kutoka kwa mastaa hao ambao kwa sasa wengi wapo kimya
wakihofia kutengwa na wazee wa ‘fitina bin Logiki’.
Awali kulikuwapo na taarifa za kuwapo
kwa msanii Matonya, ambaye hata hivyo mtandao wa Lady Jay Dee ulitoa
hadharani kuwa mwanamuziki huyo ameshachukua ‘advance’ ya shoo hiyo na
wazee wa ‘kuingilia logik’ wameshamtisha Matonya ili ajitoe, lakini
akiwa ameshatafuna pesa ya watu.
Mtandao huo wa kijamii blog,
ilinukuu kila kitu juu ya Makubaliano baina ya Capt.Gadna G Habashi na
Matonya ambapo pia unaweza kuyasoma kupitia (Ladyjaydee.blogspot.com) Pia
ulitoa kwa mara ya kwanza picha,maelezo muhimu na video ya wanamuziki
hao wawili Linah na Barnaba wakiingia mkataba wa shoo hiyo na pia
kuhamasisha watu kufika Mei 13..
**KWA TAARIFA ZAIDI KWA KINA JUU YA
BARNABA NA LINAH, usikose kuzisoma katika gazeti la Tanzania Daima **
Pindi watakapopatikana tutaweka hadharani kila kitu.


Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment