MBUNGE wa Viti Maalumu wa Chama cha
Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), Mwanamrisho Taratibu Abama jana asubuhi aliugua
na kuanguka ghafla katika viwanja
vya Bunge na kukimbizwa hospitali....
Tukio hilo lilitokea wakati akienda
kuhudhuria
semina ya wabunge kuhusu Rasimu ya Sera ya Gesi Asilia kabla ya kukosa
nguvu na kudondoka na kisha kusaidiwa na wenzake kumkimbiza kwenye
zahanati ya Bunge.
Baada ya kupatiwa huduma ya kwanza
bungeni, gari la
wagonjwa lilimkimbiza Hospitali ya Mkoa wa Dodoma (General) ambako
amelazwa.
Kwa mujibu wa waliomshuhudia, mbunge
huyo alianza kwa kuishiwa nguvu hali ambayo waliokuwa
karibu walimsaidia kumpeleka kwenye zahanati ambako alitundikiwa
dripu kabla ya kupelekwa hospitalini.
Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment