
Katherine B. O'Connor akifanya
dhihaka zake.
Mwanafunzi mmoja wa kike wa Chuo
Kikuu cha Carnegie Mellon ameshitakiwa Ijumaa kwa hali ya uvunjaji
heshima na polisi wa kampasi baada ya Askofu Katoliki kulalamika kuhusu
kutembea kwake hadharani akiwa uchi kuanzia kiunoni kwenda chini huku
kavalia kama Papa.
Mwanafunzi mmoja wa kiume ambaye
alikuwa uchi pia ameshitakiwa, lakini haikufahamika mara moja alichokuwa
akifanya wakati wa gwaride la sanaa ya uchoraji la majira ya bamvua ya
Shule ya Pittsburgh mwezi uliopita.
Rais wa Chuo hicho, Jared Cohon
alisema Ijumaa iliyopita kwamba mashitaka hayo madogo yalikuwa
yamefunguliwa huko Allegheny County dhidi ya wanafunzi hao wawili na
kwamba shule hiyo haitachukua hatua zozote zaidi za kinidhamu.
Alisema shule hiyo imebariki
kujieleza kisanii lakini kujianika uchi hadharani ni kinyume cha sheria.
"Kuna ushindani wa thamani katika
suala hapa: Carnegie Mellon inakusudia kuwa sehemu ambako mawazo
yanaweza kuwasilishwa na kujadiliwa kwa uwazi, lakini pia ambapo watu wa
historia zote, dini, na imani kujisikia wanakaribishwa na kupewa
msaada," alisema Cohon.
Askofu David Zubik wa Dayosisi
Katoliki ya Pittsburgh alilalamika baada ya gwaride hilo Aprili 18,
ambapo mwanafunzi huyo wa kike - huku nywele zake za sehemu za siri
zikiwa zimenyolewa kwa alama ya msalaba - alirusha kondomu kwa
watazamaji. Cohon aliomba radhi wiki iliyopita kwa onesho hilo.
Chuo hicho hakikuwataja wanafunzi hao
wawili. Rekodi za mahakama zinaonesha wanafunzi hao Katherine B.
O'Connor, miaka 19, kutoka Pittsburgh, na Robb S. Godshaw, miaka 22,
kutoka Wilmette, Illinois, walishitakiwa na polisi wa kampasi kwa tukio
la uvunjaji heshima. Hakuna mwanasheria aliyekuwa amejitokeza kumtetea
yeyote.
Si O'Connor wala Godshaw aliyejibu
ombi la kutoa maoni yoyote kuhusiana na suala hilo.
Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa kwa
mara ya kwanza Juni 10, mwaka huu.
Zubik alisema katika taarifa Ijumaa
kwamba Chuo Kikuu hicho kinalichukulia 'tukio hili lisilotarajiwa' kwa
uzito wa kipekee.
Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment