Wadau waliojitokeza kuishinikiza Serikali ni pamoja na kinamama kama wanavyo onekana katika picha hapo juu
Kufuatia
ajali mbili za kusikitisha zilizotokea hivi karibuni ikiwemo ajali ya
watu wawili kubanwa na magari ya mizigo kwa muda wa masaa 16 katika eneo
la maseyu, morogoro bila kupata msaada mpaka kupelekea vifo vyao na ile
ya kuanguka kwa jengo la ghorofa na kusababisha vifo vya watu zaidi ya
30, baadhi ya wawekezaji katika sekta ya usafirishaji wakiwa na mabango
wamejitokeza na kuelezea uwezo wao wa kuweza kushiriki katika kazi za
uokoaji kwa kutumia vifaa walivyo navyo lakini urasimu wa upatikanaji
vibali uliowekwa na serikali umekuwa ni kikwazo kikubwa kwao.
Wakizungumza
kwa uchungu wasafirishaji hao akiwemo mkurugenzi mtendaji wa usangu
logistics bwana Ibrahim Ismail wamesema kuwa pamoja na kuwa na magari
maalumu yenye uwezo wa kuokoa kwa haraka maisha ya watu na mali zao,
magari hayo yamekuwa hayatumiki majanga kama hayo yanapotokea kutokana
na urasimu wa upatikanaji vibali kutoka mamlaka ya barabara tanroads na
kuiomba serikali kuangalia suala hilo kiundani ili kuyaachia magari hayo
yafanye kazi bila vikwazo kwa kuwa ajali huweza kutokea muda wowote.
Aidha
wawekezaji hao wameongeza kuwa ajali za magari makubwa kuanguka
zimekuwa zikitokea mara kwa mara hususani katika barabara kuu na mara
nyingine kusababisha kukatika kwa mawasiliano ambapo wamekuwa
wakishindwa kutoa msaada kutokana na usumbufu wanao upata katika
upatikanaji wa vibali ambapo kutokana na tatizo hilo wanalazimika
kuhamishia magari hayo nchi za jirani ili yaweze kufanya kazi
yaliyokusudiwa.
Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment