Skip to main content
WABUNGE WAKERWA NA SH BILION 1 ZA KUZIKA VIONGOZI.....
Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola akichangia
mjadala wa Hotuba ya makadirio ya fedha katika Ofisi ya Waziri
Mkuu,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa mwaka wa fedha 2013/14
ambapo alitamka kutounga mkono makadirio hayo. Picha na Edwin Mjwahuzi
Ni zilizotangazwa kutengwa kupitia Hotuba
ya Waziri Mkuu.
Dodoma. Serikali ya Rais Jakaya Kikwete imelaumiwa
kwa kutenga Sh1 bilioni kwa ajili ya maziko ya viongozi huku Watanzania
wengi wakilia na umaskini mkubwa.
Shutuma hizo zilitolewa mwishoni
mwa wiki bungeni kwa nyakati tofauti wabunge akiwamo wa Viti Maalumu
Lucy Owenya (Chadema) na Kangi Lugola (Mwibara-CCM) wakati wakichangia
hotuba ya makadirio ya bajeti katika Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa
fedha 2013/14.
Katika mchango wake Owenya alisema inatia
aibu kuona kiasi kikubwa cha fedha kikitengwa kwa ajili ya maandalizi ya
kuzika viongozi huku mambo muhimu na ambayo ni kipaumbele yakiachwa.
"Ni
aibu na fedheha kubwa, hivi mmetenga kiasi hicho kwani mnajua nani
atakufa na lini atakufa ndio maana mnajiandaa kumzika," alihoji Owenya.
Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment