Waziri
Kivuli Fedha na Uchumi, Kabwe Zuberi Zitto (Mb).
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ametoa taarifa yake ya mwaka
2011/2012 na kuonyesha kuwa kuna skandali kubwa sana katika akaunti ya
Deni la Taifa. Nanukuu ‘Uhakiki wa mchanganuo wa madeni ya Taifa
kama ulivyokuwa tarehe 30
Juni, 2012 ulibaini kuwepo kwa marekebisho
ya deni ya shilingi 619,803,554,183.91 ambayo uongozi haukuweza kutoa
maelezo ya kuridhisha.’ (Taarifa
ya CAG, Ripoti ya Serikali Kuu 2011/2012 uk 158).Mwisho wa Kunukuu Katika
Taarifa yake hiyo CAG anaendelea kuonyesha kuwa Deni la Taifa linazidi
kukua na mwaka unaoishia mwezi Juni 2012 deni lilikuwa kwa asilimia 17
kutoka mwaka unaoishia mwezi Juni 2011.
Kukosekana
kwa maelezo ya kuridhisha kuhusu zaidi ya nusu trilioni za Deni la
Taifa ni jambo linalopaswa kutiliwa mashaka
makubwa, kuchunguzwa na
kupata majawabu stahiki. Tafiti mbalimbali duniani zinaonyesha kuwa kuna
mahusiano makubwa sana kati ya Deni la Taifa la utoroshaji wa fedha
kwenda kwenye mabenki ya ‘offshore’. Katika kitabu cha ‘Africa’s Odious
Debts: How Foreign Loans and Capital flight bled a continent’
kilichoandikwa mabwana Leonce Ndikumana na James Boyce imeonekana kwamba
Deni la Taifa huchochea utoroshwaji wa Fedha kwenda kuficha nje ya
Tanzania.
Mabilioni haya kwenye akaunti ya Deni la Taifa yanashtusha
sana. Kambi ya Upinzani Bungeni kwa miaka miwili mfululizo imekuwa
ikitaka ukaguzi maalumu kwenye akaunti za Deni la Taifa lakini Serikali
imeshindwa kufanya hivyo. Nikiwa Mwenyekiti wa Kamati ya PAC pia
nimemtaka CAG afanye ukaguzi huu maalumu.
Kambi ya upinzani Bungeni ilisema hivi katika Bajeti yake
kivuli 2012/13:
DENI LA TAIFA
Mheshimiwa Spika,
Kambi ya Upinzani inasikitika kwa serikali kuendelea kutengeneza madeni
kwa Taifa kwa kuendelea kukopa zaidi kwa matumizi ya kawaida ya
serikali. Wakati Serikali inasisitiza kwamba Deni letu linastahmilika,
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali anaonyesha mashaka makubwa sana
kutokana na kasi ya kukua kwa Deni la Taifa. Taarifa ya Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali inaonyesha kuwa Deni la Taifa
linazidi kuongezeka kwa asilimia 38% kutoka shilingi trillion 10.5 mwaka
2009/2010 hadi shilingi trillion 14.4 mwaka 2010/2011. Kwa mujibu wa
Waziri wa Fedha Deni la Taifa limefikia shilingi trillion 20.3 mpaka
ilipofika mwezi Machi mwaka 2012. Ukisoma taarifa ya Mwezi wa Mei 2012
ya Benki Kuu ya Tanzania, Deni la Taifa sasa limefikia shilingi trillion
22.
Mheshimiwa Spika, Suala hapa sio
ustahmilivu wa Deni kama inavyodai Serikali bali ni kwamba tunakopa
kufanyia nini? Bajeti ya
Mwaka 2012/13 inayopendekezwa inaonyesha
kwamba Serikali itakusanya shilingi trilioni 8.7 kama makusanyo ya ndani
na itatumia shilingi trilioni 10.6 kama matumizi ya kawaida. Ni dhahiri
kwamba sehemu ya mikopo ambayo serikali inachukua sasa itakwenda kwenye
matumizi ya kawaida. Hatutaki mikopo kwa ajili ya matumizi ya kawaida
ya posho, kusafiri, magari nk. Tuchukue mikopo kuwekeza kwenye miradi
itakayokuza uchumi na kuzalisha kodi zaidi. Bajeti inaonyesha kwamba
Serikali itakopa shilingi takribani trillion 5 mwaka 2012/13. Serikali
ikubalikutekeleza mapendekezoya Kambi ya Upinzani ya kuimarisha
ukusanyaji wa kodi na kupanua wigo wa kodi katika maeneo muhimu kama
sekta ya madini na mawasiliano, kuzuia misamaha ya kodi, kutokomeza
ukwepaji kodi, na kuepuka matumizi mabaya ili kuepuka madeni yasiyo ya
lazima.
Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani
inapenda kusisitiza kwamba Bunge lifanye ukaguzi maalumu kuhusu akaunti
ya Deni la Taifa ili kuweza kubaini ukweli kuhusu ustahmilivu wa Deni na
mikopo ambayo Serikali inachukua kama inakwenda kwenye Maendeleo na
miradi ipi na kama miradi hiyo ina tija. Vilevile tumependekeza kwamba
Mikopo yote ambayo Serikali inachukua iwe inapata idhini ya Kamati ya
Bunge ya Fedha na Uchumi au Bunge litunge sharia ili kiwango cha juu cha
kukopa ambacho Serikali haipaswi kuvuka. Kuiacha Serikali inaendelea
kukopa bila mpango ni kuliweka Taifa rehani na kupeleka mzigo wa kulipa
madeni haya kwa kizazi kijacho. Hatuwezi kukubali Wazee wetu waishi
maisha yao, waishi maisha yetu na pia wakope maisha ya watoto wetu.
Mwisho wa kunukuu.
Kambi ya Upinzani inarejea kutaka ukaguzi maalumu kuhusu
akaunti za Deni la Taifa na maelezo ya kina ya Serikali kuhusu shilingi
620 bilioni ambazo hazina maelezo kwenye Deni la Taifa.
Hatuwezi
kukaa kimya kuona Watanzania wanabebeshwa madeni ambayo kimsingi ni
madeni bandia yanayotajirisha watu wachache wenye uwezo na ujasiri
mkubwa wa kuiba, kupora nakufisidi hazina ya Taifa letu.
Waziri Kivuli Fedha na Uchumi, Kabwe Zuberi Zitto (Mb)
Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment