Zaidi ya abiria 100 wamenusurika
kimiujiza jana baada ya ndege kuvuka njia ya kutua/kuruka na kwenda hadi
ufukwe wa Bali na kujikita kwenye bahari.
Mashuhuda walisema abiria
waliokuwa wakihofia maisha yao walipiga makelele kutokana na
kuchanganyikiwa huku ndege hiyo ya Lion Air ilipovuka njia ya
kutua/kuruka kwenye Uwanja wa Ndege wa Ngurah Rai, karibu na Denparsar.
Ndege hiyo, ilikuwa imebeba abiria 101
na wafanyakazi saba - kisha ikatumbukia baharini kutoka urefu wa karibu
mita 50 juu.
Abiria waliojawa na hofu
walipigwa picha wakitoka kwenye ndege hiyo iliyovunjika vipande, huku
wengi wakisubiri juu ya mabawa yake wakati waokoaji wakifanya juhudi za
aina yake za ukoaji.
Uwanja huo wa ndege unafahamika
zaidi kutokana na njia yake ya kuruka/kutua kurefushwa hadi
baharini.Wengi wa abiria waliokoka kupitia milango ya dharura ambayo
ilifunguliwa nusu sambamba na kiunzi hicho cha ndege na kufanya njia yao
kuelekea ufukweni.
Baada ya kuwa wameokolewa kutoka
kwenye ndege, walipelekwa kwenye uwanja wa ndege kwa ajili ya kupatiwa
matibabu.
Maofisa wa Uwanja wa Ndege walisema
kwamba watu kadhaa walijeruhiwa kwenye ajali hiyo, lakini ukubwa wa
majeraha yao haukuweza kufahamika.
Lion Air kwa sasa imefungiwa kusafiri
katika Umoja wa Ulaya sababu ya hofu kuhusu viwango vya usalama wake.
Mkuu wa Polisi Bali, Arif Wahyunadi
alisema: "Abiria wote na wafanyakazi wameondolewa kwenye ndege hiyo huku
ikiwa imelala kwenye maji.
"Wamepokelewa na kuhudumiwa kwenye
uwanja wa ndege."
Abiria wote
na wafanyakazi wameokolewa salama na kwamba watu 22 wamepelekwa kwenye
hospitali tatu tofauti kutokana na majeraha mbalimbali.
Taarifa za awali zinaonesha kwamba
kulikuwa na abiria 101 na wafanyakazi saba ndani ya ndege hiyo.
Wahyunadi alisema ndege hiyo asili
yake ni mji wa Bandung, mji wa tatu kwa ukubwa nchini Indonesia -
kivutio cha utalii sababu ya ujenzi wake.
KUHUSU SHIRIKA LA NDEGE LA LION AIR:
Ndege ilikuwa ikimilikiwa na Lion Air, ambalo
kaulimbiu yake ni: Tunawezesha Watu Kuruka.Ni shirika la ndege binafsi
la pili kwa ukubwa nchini Indonesia, likishikilia sehemu kubwa ya soko
la ndani.
Shirika hilo linafanya safari
zake kwenda miji mikuu ya Indonesia, na pia safari nyingine Kusini
Mashariki mwa Asia, ikichukua abiria kwenda Vietnam, Singapore, Malaysia
na hata Saudi Arabia. Likianzishwa mwaka 1999, shirika hilo lilianza
kutumia ndege moja aina ya Boeing 737-200.
Lion Air ni ndege zinazotoza
viwango vya chini vya nauli ambalo linashikilia asilimia 45 ya soko
nchini Indonesia.
Lion Air limesaini mkataba wa Dola za
Marekani bilioni 24 mwezi uliopita kwa ajili ya kununulia ndege 234 aina
ya Airbus, oda kubwa kabisa kuwahi kupokewa katika karakana ya kuunda
ndege nchini Ufaransa. Pia ilitoa oda kubwa kabisa kwa Boeing pale
ilipokamisha mkataba wa kununua ndege 230 mwaka jana. Ndege hizo
zitaanza kukabidhiwa kwa Lion Air kuanzia mwaka 2014 hadi 2026.
Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment