Skip to main content
MLELA ADAIWA KUMTUNDIKA DENTI MIMBA NA KUMKANA.....
STAA wa filamu za Kibongo, Yusuph Mlela amedaiwa kumtundika mimba
mwanafunzi aliyefahamika kwa jina moja la Salha, mkazi wa Zanzibar
ambaye anasoma katika chuo cha ITF, Tandika, jijini Dar.
Kwa mujibu wa chanzo makini kilichoomba hifadhi ya jina
lake kilichopo chuoni hapo, Mlela alidaiwa kuwa na uhusiano wa
kimapenzi na denti huyo kwa muda mrefu ambapo mashosti wote wa Salha,
walikuwa wakimtambua kama shemeji yao hadi alipodaiwa kumpa kibendi.
“Unajua shemeji yetu (Mlela) alikuwa anakuja sana hapa chuoni lakini
baada ya kuambiwa yule Salha ana ujauzito wake, aliruka viunzi na kusema
hahitaji mtoto, atoe mimba.
“Salha alipokataa ndipo Mlela alipoamua
kukata mguu kabisa, tukawa hatumuoni,’’ kilisema chanzo hicho.
Alipotafutwa Mlela kuhusiana na ishu hiyo, alimkana mwanafunzi huyo na
kusema hamtambui na wala chuo anachosoma hakijui.
“Huyo msichana
simjui hata hicho chuo chenyewe cha Tandika sijawahi kufika huko, kama
huyo binti ana ushahidi auweke hadharani,’’ alisema Mlela.
Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment