aah kusema ukweli kitu kikubwa
kinachotokea ni kwamba, imefika kipindi sasa imebidi wasanii wa Tanzania
inabidi tuamke tuone wapi tunataka tuelekee na pia tuanza kutafakari ni
wapi mziki wetu tunataka uelekee, kwasababu tumefanya mziki huu kwa
mafanikio, tumetoka mbali kwenye sehem za hatari sana na sasa tuna
advantage ya kwamba kiswahili kiswahili kinaenda kama lugha ya kimataifa
tumepata mashabiki nje ya tanzania.....".
ndio maana leo kwenye account yangu
ya twitter nikasema, inafika kipindi sasa tuangalie, kwasababu kila
mmoja anakua anamtupia lawama mwenzake na vitu vingine kama hivi, ni
kwamba tukae kama wasanii kama watanzania tunaotaka tuangalie mziki huu
tunataka tuupeleke wapi....
kiukweli inavyoonekana anaeuharibu
mziki huu sio mtu mmoja....wasanii kama wasanii unakuta wanaandika
mashairi ambayo hayaeleweki hata kwenyejukwaa perfomance zao vingine
havisaidii kuupeleka mziki wetu mbali hata media inaonekana kucheza
nyimbo zingine ambazo kiulweli kabisa hazisaiidii chochote kwenye mziki
wetu wa Tanzania na katika harakati hizi za kuupeleka mziki wetu
kwenye level, "
"lawama zangu pia nazipeleka kwa
mashabiki, kwasababu wana nyimbo zao ambazo wanapioga simu wanaomba,
kwenye matamasha wanasapoti ya watu wengine lakini kiukweli zile nyimbo
hazisaidii chochote, mashabiki saa zingine wanaomba nyimbo ambazo
hazisaidii chochote na zinakuwa mbovu, "
"lakini kitu ambacho kikubwa kabisa
cha mwisho, ni kwamba serikali ina play part vipi katika swala hili,
ikiwa kama baba wa watanzania wote inabidi itoe kauli,kwasababu wasanii
kila siku kilio chao ni kwamba kazi zao zinaibiwa watu wanakosa ubunifu
ndio maana wanaimba vitu ambavyo viko bubble gum, na vitu ambavyo
havieleweki, serikali kama serikali ingejaribu kuangalia jinsi gani ya
kuwasaidia wasanii wa Tanzania especially katika kazi zao, kwenye vitu
kama ringtones, lakini pia katika sheria jinsi gani msanii anaweza
kunufaika na kazi zake anayoifanya, kwasababu hata sasa hivi hizi stika
za TRA haziwezi kusaidia kitu stika zitakuwepo lakini tatizo sugu
tumeliacha, tatizo ni wizi wa kazi za wasanii......." amesema Prof Jay
|
Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment