FARAJA KOTA, MUMEWE KAMA OBAMA NA MICHELLE......

REMBO aliyewahi kushika Taji la Miss Tanzania, Faraja Kota na mumewe Mheshimiwa Lazaro Nyarandu wamefananishwa na Rais wa Marekani, Barak Obama na mkewe Michelle Obama kutokana na muonekano wao

Hivi karibuni mtandao wa 8020 fashion, ulitupia picha za Faraja na mumewe  wakiwa wameongozana kwenye hafla ya uzinduzi wa mtandao wa www.shlendrect.co.tz ambapo wawili hao walionekana wakishikana mikono kama wafanyavyo Obama na mkewe.

Kupitia mtandao huo, watu walitupia maoni na kusema kuwa  wanandoa hao maarufu wanapaswa kuigwa na watu maarufu wote kwani wamewafananisha na Rais Obama na mkewe ambao wana heshima kubwa katika jamii.

Comments