Zaidi ya kesi 21, 000 za maambukizi mapya
zimedaiwa kutambulika kwa mwaka 2011/12.
Kondomu hizo feki aina ya Trojan na Durex
zenye vipele vipele ambazo
mwishoni mwa mwaka jana serikali ya Uingereza iliingia katika msako
mkali kusaka mamilioni ya kondomu hizo bandia zilizokuwa zikiuzwa nchini
humo miezi 18 iliyopita.
Kirusi kinachoambukiza ugonjwa huo hatari
kimetajwa kuwa ni
'Neisseria' ambacho ni tofauti na vingine ambavyo mara nyingi hutibiwa
kwa dozi moja tu ya viuavijasumu (antibiotics) ambayo angalau hufanya
kazi kwa asilimia 95 kiufanisi.
Akizungumzia maendeleo ya utafiti wa kondomu
hizo nchini , Kaimu
Mkurugenzi wa Shirika la Wiwango Tanzania(TBS),Leandri Kinabo alisema
shirika hilo kwa kushirikiana na Mamlaka ya Ckula na Dawa(TFDA) hivi
sasa lipo katika mchakato wa kuhakikisha vipimo halisi vya ubora wa
bidhaa hizo vinaangaliwa.
"Hili suala
ni nyeti na ni la kiafya na usalama zaidi, hivyo tulikaa
kikao na TFDA na tulikubaliana tufanye uchunguzi wa kondom hizi, kwani
ni kweli zipo sokoni lakini suala la ubora linatakiwa kuangaliwa,"
alisema Kinabo.
Aliwataka Watanzania kuwa na subira ili
waweze kuchunguza bidhaa hizo
kwa umakini zaidi na kwamba baada ya uchunguzi watatoa majibu.
Baada ya gazeti hili kutaka kujua uhalali wa
bidhaa hizo sokoni,
Kinabo alisema bidhaa zote zinazoingia bandarini hupimwa, lakini kuna
baadhi ya bidhaa ambazo huingizwa kwa njia zisizo halali na mara nyingi
huwa feki.
"Inetegemea na
lebo ya bidhaa husika, kuna wakati bidhaa inaweza
kupimwa na kuonekana kuwa ni salama na kisha kuingizwa sokoni, lakini
baada ya muda zikaingia bidhaa feki zenye nembo hiyohiyo, hivyo hilo ni
suala la kusubiri vipimo kutoka TFDA," alisema Kinabo.
Tatizo hilo sugu Uingereza limesababishwa
kuanzishwa kwa kampeni mpya
ya kukabiliana na tishio kubwa la kuongezeka kwa kasi kwa magonjwa hayo
nchini Uingereza na Wales ambayo yamedaiwa kusambaa kwa wingi nchini
humo na nchi zinazoendelea.
Wataalamu wa Afya wana matumaini mapya baada
ya kuanzishwa mpango
mkakati wa kuzuia ugonjwa wa gono 'Gonorrhoea Resistance Action Plan'
ambayo itaongeza ufahamu wa ugonjwa huo.
Mpango huo ulioanzishwa na shirika la Ulinzi
wa Afya, utafuatilia
tatizo hilo la kimataifa linaloongezeka kwa kasi tangu kupungua miaka 10
iliyopita.
Tatizo hili limeanza kukua kwa kasi mwaka
2011, wagonjwa wengi
waliojitokeza wameugua zaidi ya mara tatu magonjwa ya ngono. Zaidi ya
theluthi ya kesi hizi ni za wanaume waliokuwa wakifanya mapenzi na
wanaume wenzao, kutoka karibu ya robo kwa mwaka 2010.
Profesa Cathy Ison kiongozi wa kampeni hiyo
anasema "idadi kubwa ya
watu waliougua magonjwa haya wanatamka kuwa walipata kutumia kondom
ambazo hata hivyo baadaye zilitambulika kuwa ni feki na kuzuiwa hapa
nchini Uingereza.
"Bado hatuwezi
kuwahakikishia watu kuwa tunatarajia kupata suluhu ya
gono hili hatari, hili bado ni tatizo kubwa kwa afya ya umma na ni
kwamba sasa limeanza kusambaa hata nchi zinazoendelea,"
anasema Ison.
Nchini Uingereza na Wales, kuna hatari kubwa
ya kuendelea kwa
maambukizi haya ambayo hata hivyo yameonekana kukua kwa kasi kubwa licha
ya wagonjwa wengi kudai kuwa hutumia mipira katika tendo la kujamiiana.
Ingawaje kesi za kushindwa kutibu gono hilo
zimekuwa ni taarifa za
kimataifa, Afisa Mganga Mkuu Uingereza, Profesa Sally Davies, hivi
karibuni aliishauri serikali kuongeza nguvu katika dawa za Antibiotics
kwa ajili ya dharura kwa wagonjwa watakaopatikana na gonjwa hilo.
Prof esa Davies anasema "tumeona na kuwa na wasiwasi mkubwa katika
kesi za dawa sugu za magonjwa ya zinaa kwa muongo uliopita, lakini kuna
haja ya kutengeneza dawa hizo kwa ajili ya tatizo hili, labda
tutafanikiwa, lakini kazi ya ulinzi wa shirika la afya ni muhimu katika
kutafuta suluhu ya tatizo hili" anasema.
Mdhibiti wa dawa na bidhaa za afya nchini
humo, alidai kwamba
mamilioni ya kondom hizo feki ziliingia nchini humo zikitokea Mashariki
ya Mbali na kwamba zimeshatumiwa na watu wengi tangu kuingizwa nchini
humo.
Kondom hizo zilidaiwa kutengenezwa kwa vifaa
rahisi visivyo na ubora
ambavyo vinaweza kuongeza hatari kwa watumiaji kwa kusambaza kwa kasi
magonjwa ya zinaa, au kusababisha mimba zisizohitajika, pamoja na
kuharibu mikakati ya uzazi wa mpango.(Herrieth Makwetta)
Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment