Skip to main content
ROSE NDAUKA AROGWA ILI ASIFANIKIWE NA APOTEZE MVUTO KWA JAMII........
STAA wa filamu za Kibongo, Rose Ndauka amedaiwa kurogwa ili
asifanikiwe na kupoteza mvuto kwa jamii.
Chanzo chetu makini kwa sharti la kuchorwa jina lake kilimtonya paparazi wetu kuwa, staa huyo mwenye sura yenye mvuto
amerogwa na wasanii wenzake ambao hawapendi mafanikio yake na ndiyo
maana anakosa dili nyingi za kushuti kama zamani.
“Mara kwa mara amekuwa akipewa taarifa za kurogwa lakini yeye amekuwa
akizipotezea sasa shauri yake, atapotea,” kilisema chanzo hicho.
Alipoulizwa juu ya taarifa hizo za kuwa anarogwa, Rose alisema yeye
haamini ushirikina ila alikiri kupokea taarifa hizo kutoka Zanzibar
lakini maisha yake amemuachia Mungu.
“Nimekuwa nikipuuza habari hizi kwani nimezisikia sana, juzi
nilipigiwa simu na mtu mmoja aliyedai anaishi Zanzibar na kuniambia kuna
msanii alikwenda kunimaliza kishirikina hivyo kama ninataka kupona
nimfuate kisiwani humo lakini mimi sikwenda ingawa kidogo nimekosa
amani,” alisema Rose.
Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment