MSANII REAL JOFU ATANGAZA UJIO WAKE MPYA KWENYE MZIKI

Msanii Real Jofu aliyewai kutamba na ngoma yake ya Verifa iliyowahi kufanya vizuri kwenye anga za bongo, amewaambia mashabiki wake wakae mkao wa kula kwani kwa sasa amejiandaa vya kutosha sana tu.



Akiongea na SHEBBY D BLOG amesema kukaa kwake kimya ni kwa ajili ya masomo yalikuwa yanambana nasasa yupo safi kwani amesema amesharekodi nyimbo nne ambazo kwa sasa yupo kweye maandalizi ya kuzifanyia video zote ndipo atapozitambulisha rasmi. Amewaomba mashabiki wake mkao wa kula kwani vitu vinakuja vikali tena babu kubwa. 

SHEBBY D BLOG inamtakia maandalizi mema Real Jofu.

Comments