Skip to main content
Mchungaji aumbuliwa na changudoa
KAMA unaamini wachungaji wote watakwenda peponi basi utakuwa
unakosea. Hebu sikia hii. Mchungaji mmoja aliyejulikana kwa jina la
Michael Njoroge kutoka nchini Kenya amekumbwa na skendo nzito baada ya
mwanamke mmoja ambaye ni changudoa kuibuka hadharani na kudai
alinunuliwa na pastor huyo kwenda kanisani kutoa ushuhuda wa uongo,
Amani limeinyaka.
Kwa mujibu wa mitandao mbalimbali ya nchini humo,
kahaba huyo aliyejitambulisha kwa jina la Ester Mwende, awali alifuatwa
na mtumishi huyo wa Mungu na kumtaka wafanye mapenzi zoezi ambalo
lilifanyika.
Akasema baada ya zoezi hilo, ndipo mtumishi huyo wa
Kanisa la Fire Ministries Embakasi alimtaka afike kanisani hapo ili
kutoa ushuhuda wa uongo na kumuahidi kwamba angemlipa kiasi cha shilingi
10,000 za Kenya (kama 180, 000 za Tanzania).
Mwande ambaye alikuwa
akitoa ushuhuda huo kwenye Kituo cha NTV cha nchini humo, alisema
alikubali na kesho yake alikwenda kanisani kwa mchungaji huyo
anayesifika sana kwa miujiza na upako.
Akasema: Nilipofika nilikaa na kujifanya nimepinda midomo. Muda wa
maombezi mchungaji akasimama na kusema mimi nina matatizo, nimepinda
midomo kwa sababu kuna kanisa nilikwenda nikasema kuna mchungaji amebaka
mtu kwa hiyo pigo langu lilikuwa kupinduka midomo.
Mwande aliendelea
kusema kwamba mpaka anatoka kanisani hapo bado alikuwa amejipindisha
midomo jambo lililomfanya kila mtu aliyemuona aamini.
Akasema kesho
yake alirudi tena na muda wa watu kushuhudia uponyaji, yeye alitoka
mbele. Mchungaji alipomwona aliwaangalia watu na kuwaambia: Huyu mama ni
yule aliyekuja jana akiwa amepinduka midomo kwa sababu ya kuwasema
vibaya watumishi wa Mungu.
Mwande alisema alishuhudia kwamba baada ya
maombezi ya siku iliyopita anamshukuru Mungu alimponya na midomo yake
iko sawasawa kama zamani, kauli iliyosababisha kanisa zima kulipuka kwa
shangwe za kumtukuza Mungu.
Mwande alisema aliamua kuweka wazi madai hayo baada ya mtumishi huyo
kumrusha fedha nyingine walizokubaliana akidai kwamba mbali na yeye pia
mchungaji huyo alimtaka amtafutie makahaba wengine watatu, jambo ambalo
alilitekeleza lakini nao pia hakuwalipa.
Makahaba wenzake Mwande, wao
walisema walimtumikia mtumishi huyo kwa kutoa shuhuda za uongo lakini
hakuwalipa ujira wao na walipomfuata aliwajeruhi miguuni.
Walisema baada ya tukio hilo, walitoa ripoti kwenye Kituo cha Polisi
cha Embakasi lakini maafande hao walikuwa wakisuasua kumtia mbaroni
mtumishi huyo.
Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment