Skip to main content
Watuhumiwa Mara wawaua wanaoipinga uvuvi haramu.
Watu wawili wameuawa kwa kupigwa na makasia na mawe baada ya kuwazuia
wavuvi watatu kuvua samaki kwa kutumia sumu katika ziwa Viktoria.
Tukio hilo limetokea katika kijiji cha Kiyemba kata ya Nyakande
wilayani Butiama mkoani Mara.
Waliofariki wametajwa kuwa ni Sanya Rwanya mkazi wa Kijiji cha Kiemba
na Kingi Magesa mkazi wa kijiji cha Kabegi kata ya Nyakatende.
Diwani wa kata hiyo Mheshimiwa Jerald Kasonyi amesema vitendo vya
uvuvi haramu vimekithiri katika kata hiyo jambo ambalo limesababisha
wavuvi haramu kutumia fursa iliyopo kufanya shughuli zao bila vificho
hali inayochangia wananchi kijaribu kupambana nao.
Ameongeza kuwa alipata taarifa za tukio hilo la kuuawa kwa watu hao
kuwa wavuvi wawili wameuawa na wavuvi haramu wa kutumia sumu hali
iliyomlazimu kuwasiliana na uongozi wa jeshi la polisi ili uweze
kuwasaidia.
Mwenyekiti wa kijiji hicho Aliphonse Magati amesema vitendo hivyo
vimekuwa vikiwaogopesha wananchi wa kijiji cha Kihemba kufanya shughuli
za uvuvi na kuongeza kuwa serikali iwasaidie katika kukabiliana na
matukio ya uvuvi haramu kijijini humo.
Nao wananchi wa vijiji hivyo wameiomba serikali kuwahakikishia
usalama wao kwa kuweka doria katika maeneo mbalimbali ya Ziwa Viktoria.
Vitendo vya uvuvi haramu vimekithiri kwa kiasi kikubwa katika ziwa
ViKtoria mkoani Mara hali inayoelezwa na wavuvi kuwa ni kushindwa kwa
kikosi cha kupambana na wavuvi haramu mkoani humo kufanya doria za mara
kwa mara.
Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment