
MAMA Mzazi wa msanii nyota Tanzania marehemu
Steven Kanumba ‘Kanumba’
Frola Mtegoa ameigiza filamu katika muendelezo wa kipaji cha mwanaye
baada ya kuigiza katika filamu ya Without
Daddy akishirikiana na watoto
waliokuwa wakiigiza na marehemu Kanumba kama Patrick na Jamila, katika
filamu hiyo mama Kanumba kaigiza katika kiwango cha juu.
.
Ben Blanco
akiwa na wasanii wakali Jamila na mwenzake.
Akiongea na FC mkurugenzi wa kampuni ya Big
Daddy Production Irene
Kaungwa amesema kuwa filamu ya Without
Daddy ni kazi mwendelezo wa kazi
ya marehemu Kanumba iliyotoka siku za nyuma ya Big Daddy na ni kazi
ambayo imetentengezwa kwa ubora wa kimataifa ikiwa sambamba na
kumtambulisha mama Kanumba katika tasnia ya filamu Swahiliwood.
“Kampuni ya Big Daddy Production imekusudia kuleta mapinduzi makubwa katika tasnia ya filamu Tanzania, na katika kumuenzi marehemu tumemchukua mama Kanumba kushiriki katika filamu hiyo na mama ameonyesha uwezo mkubwa katika uigizaji na filamu yake ya kwanza
ndio hii,”anasema mkurugenzi.
.
Mmoja kati ya
wasanii walioshiriki katika Filamu ya Without Daddy.
Mama Kanumba
mwigizaji.
Filamu ya Without Daddy imeshirikisha
wasanii nyota wengi kama
vile Abdalah Mkumbilah ‘Muhogo mchungu’, Fatuma Makongoro ‘Bi. Mwenda’
Cathy Rupia, Mayasa Mrisho, ‘Maya’, Othuman Njaidi ‘Patrick’ Wastara
Juma ‘Stara’ Abdul Ahmed ‘Ben Blanco’ na wasanii mahiri wengineo.
.
“Kampuni ya Big Daddy Production imekusudia kuleta mapinduzi makubwa katika tasnia ya filamu Tanzania, na katika kumuenzi marehemu tumemchukua mama Kanumba kushiriki katika filamu hiyo na mama ameonyesha uwezo mkubwa katika uigizaji na filamu yake ya kwanza
ndio hii,”anasema mkurugenzi.
.
Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment