Skip to main content
Lowassa: Kikwete, unda Tume kuchunguza Matokeo mabaya ya Kidato cha Nne
Wakati huo huo Mh. Lowassa amemsifu kijana aliyemchora Messi na kusema
kijana huyo ni intelligent. Amesifu uwezo wa kijana huyo kufanya hivyo!
Vilevile Mh. Lowassa, ameitaka serikali kuongeza uwekezaji katika elimu
kwani amesema tofauti na nchi nyingine za Afrika Mashariki, Tanzania
ndio ya mwisho kwa uwekezaji kwani inawekeza asilimia moja point
something ya GDP katika elimu wakati Kenya ni asilimia tano na Rwanda
kama sikosei amesema inawekeza mpaka asilimia 7 ya GDP katika elimu na
hivyo ametoa wito kwa serikali kuongeza uwekezaji katika elimu.
Mh. Lowassa pia amemsifu Rais Kikwete kwa kufanikiwa katika maeneo
mengine kama ujenzi wa barabara, hospitali, zahanati na kwenye maeneo
mengine na kumtaka ajielekeze zaidi katika elimu. Mh. Lowassa amerudia
kauli yake na kusisitiza kuwa msimamo wake utabaki kuwa ni elimu kwanza
na sio kitu kingine.
Miongoni mwa viongozi waliohojiwa ni pamoja na Zitto Kabwe ambaye mbali
na kushauri mambo mbalimbali pia amewataka waziri wa elimu na naibu wake
pamoja na katibu mkuu wa wizara ya elimu kujiuzulu. Source: Clouds FM mchana huu.
Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment