Skip to main content
Katiba mpya, MAT wataka viongozi kutotibiwa nje.
Chama cha Madaktari Tanzania MAT kimeshauri kuwepo na kipengele
katika katiba mpya ambacho kitasitisha udhamini na matibabu ya viongozi
nje ya nchi.
Chama hicho pia kimeshauri kuondolewa adhabu ya kifo na kupiga
marufuku utoaji mimba nchini.
Ni zamu ya Madakatari kutoa maoni yao mbele ya Tume ya maoni ya
katiba mpya katika utaratibu wake wa kukutana na makundi maalum.
Dokta Primus Saidia ni Rais wa MAT anasema kuondolewa kwa kipengele
hicho kutatoa nguvu kwa serikali kustawisha Sekta ya Afya na hivyo kuwa
na fursa ya kutoa tiba za kada zote nchini.
Anasema fedha hizo zitasaidia kusomesha madaktari bingwa kukidhi
hitaji na vifaa vya kisasa vya tiba badala ya kuendelea kutegemea huduma
za kitabibu kutoka nje ya nchi.
MAT pia wameitaka tume ya marekebisho ya katiba kuangalia vipaumbele
vya kitaifa kama afya, elimu, ardhi na ustawi wa jamii na miundombinu
ili vitungiwe sheria itakayotoa usimamizi madhubuti.
Tume ya katiba ipo katika mchakato wa kupokea maoni tofauti
yatakayoingizwa kwenye katiba mpya kabla ya kujadiliwa katika mabaraza
ya kati ya Wilaya katika hatua inayofuata.
Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment