‘Addicted hit maker’ Hussein Machozi
amefunguka kuhusu
uhusiano wake na Diamond platnumz na kuonesha kuwa hawana urafiki hata
kidogo,
japo hakusema moja kwa moja kama wana uadui na kwamba yeye na Diamond ni
kama
‘Jogoo na kuku Jike’ na yeye Hussein ndiye jogoo!
Hussein Rashid a.k.a Hussein Machozi
amefunguka kwenye XXL
ya Clouds fm katika segment ya U Heard, alipotakiwa kutoa ufafanuzi
kuhusu
tuhuma zilizowafikia ‘Timu Makorokocho’ kuwa Hussein Machozi alipigana
na
Diamond Platinumz huko Mombasa.
Japo Hussein alikiri kuwa anauwezo wa
kupigana kama bondia,
lakini alikanusha kabisa kuwa hajawahi kupigana na Diamond na wala
hajawahi
kuzinguana nae, kwa sababu hawajawahi kabisa kuwa karibu, na sababu ni
kwamba
wanatokea katika sayari tofauti kabisa, yeye anatokea sayari nyingine na
hajui
Diamond anatokea sayari gani.
Japo aliongea kwa ufupi sana lakini hii
ilitoa picha ya moja
kwa moja kuwa inawezekana Hussein ana kitu moyoni ama hasira flani
kuhusu
Diamond Platinumz. Je wewe unamtazamo gani kuhusu hili?
Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment