Skip to main content
CHADEMA champa siku 14 Waziri Kawambwa kujiuzulu
Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimetoa siku 14 kwa Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dokta Shukuru Kawambwa kujiuzulu kutokana
na matokeo mabovu ya mtihani wa kidato cha nne.
Kauli hiyo inatolewa siku moja baada ya baraza la mitihani la taifa
NECTA kutangaza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2012 ambapo asilimia
sitini ya wanafunzi wote laki tatu na 67 elfu 750 waliofanya mtihani
wamefeli.
Katika Viwanja vya Furahisha jijini Mwanza Mwenyekiti wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe akiwahutubia wafuasi wa
chama hicho na wananchi anasema matokeo hayo yanatokana na mfumo mbovu
wa elimu nchini na kuwa ishara na watoto wa maskini kuendelea kukosa
elimu thabiti..
Wabunge wa Chama hicho wamesema kupingwa kwa hoja ya Mbunge wa
kuteuliwa Mheshimiwa James Mbatia ni wazi kuwa Tanzania haiwezi kupiga
hatua katika Sekta za elimu na afya.
Changamoto hiyo ya kielimu imezungumzwa katika ufunguzi wa sera ya
majimbo nchi nzima huku chama hicho kikiunda kanda 10 lengo likiwa ni
kuimarisha utawala kuanzia ndani ya chama hicho ili kuleta sera ya
mgawanyo wa rasilimali nchini.
Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi James Mbatia
amesema unahitajika mjadala wa kitaifa kuhusu kiwango na mfumo wa elimu
nchini.
Anasema serikali ina wajibu wa kuunda Tume maalum itakayoainisha kero
ambazo umma wa watanzania utazijadili ili kujenga mfumo mpya wa elimu
ya Tanzania.
Siku moja baada ya Waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Dokta Shukuru
Kawambwa kutangaza matokeo ya kidato cha nne, viongozi wa kisiasa na
wazazi wanatoa mapendekezo ya kurejesha kiwango cha elimu nchini baada
ya kushtushwa na kiwango cha ufaulu.
Mwenyekti wa Chama cha NCCR mageuzi ambaye ni Mbunge wa kuteuliwa
Mheshiwa James Mbatia anaona suluhu ya haraka ni mjadala wa kitaifa na
kuundwa Tume maalum itakayoshughulikia suala la elimu.
Susan Lyimo ni Waziri kivuli wa elimu na mafunzo ya ufundi kutoka
CHADEMA anasema kushuka kwa elimu nchini ni matokeo ya kutothaminiwa kwa
mwalimu na kuwepo kwa mfumo usiokidhi mahitaji.
Takwimu zinaonyesha kuwa ni wanafunzi 1,641 pekee waliofaulu kwa
kiwango cha daraja la kwanza huku wanafunzi waliopata Sifuri wakiwa ni
zaidi ya laki mbili na elfu 40 sawa na asilimia 60.
Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment