Skip to main content
BAADA YA KUPATA DEMU MPYA JOKEKI ATOA BARAKA KWA DIAMOND
BAADA
ya Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kupata demu mpya, Penniel Mungilwa
‘Penny’, Jokate Mwegelo ametoa baraka zake kwa jamaa huyo aliyewahi
kudaiwa kuwa mpenzi wake akisema haoni tatizo wawili hao kuwa pamoja
kama kweli wamependana na kuridhiana.
Nasibu
Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na aliyewahi kudaiwa kuwa mpenzi wake,
Jokate Mwegelo. Katika mahojiano maalum alipobanwa
kuhusiana na uhusiano wa wapenzi hao huku ikifahamika kuwa Penny alikuwa
shosti wake, Jokate ambaye ni Miss Tanzania namba 2, 2006/07 alisema
kwamba yeye na mrembo huyo walikuwa washikaji tu na wala hawakuwa na
urafiki wa karibu kama baadhi ya watu wanavyoamini.
Nasibu
Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na demu wake mpya, Penniel Mungilwa
‘Penny’.
Jokate ambaye pia ni mtangazaji wa Runinga
ya Channel O alifunguka kuwa anawatakia kila la heri na baraka zote
Diamond na Penny katika uhusiano wao mpya wa kimapenzi endapo tu
watakuwa wamependana na kuridhiana kwa dhati.
“Japokuwa sipendi
kumuongelea Diamond lakini ukweli sioni tatizo kwa wao kupendana, mimi
naona poa tu,” alifunguka Jokate ambaye pia ni bonge la mwigizaji.
Kabla
ya kutoka kimapenzi na Penny ambaye naye ni mtangazaji wa Runinga ya
DTV, Diamond aliwahi kuviteka vyombo vya habari akiripotiwa kuwa na
Jokate, kabla ya mambo kwenda mrama.
Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment