VING’AMUZI BADO CHANGAMOTO JIJINI DAR ES SALAAM

SHEBBY D BLOG


Wakati Tanzania imeingia rasmi katika mfumo mpya wa kurusha na kupokea matangazo ya Televisheni,baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wamesemamfumo huo unakabiliwa na changamoto nyingi. Katika mahojiano mahojiano maalum, baadhi ya watumiaji hao ambao wamesema kuwa wananchi hawakujiandaa vilivyo kukabiliana na changamoto.

Wananchi wamesema kuwa tatizo kubwa la baadhi ya ving’amuzi ni kukatakata na kuganda kwa picha wakati matangazo yanaendelea kitu ambacho wengi hawakutarajia. Wananchi hao wamesema hata kama kuna chaneli za bure lakini kuna changamoto kubwa ya  gharama za kununua ving’amuzi na vifaa vinavyoambatana katika kufanya kazi kwake.

Katika mitaa mbalimbali mwandishi ameshuhudia mamia ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakihaha kusaka ving’amuzi katika maduka yanayouza bidhaa hiyo muhimu kwa sasa.

Comments