Mwanamke
huyu alijitambua vyema na kukiri ndani ya nafsi yake kuwa hawezi
kuolewa na maname yoyote yule maana jamii yote ilikuwa inamtambua
kwa uchangudoa wake......
Kwa hiyo ,
ili kurahisisha mambo na kuifanya biashara yake iimarike, mwanadada
huyu aliamua kwenda hospitali kukitoa kizazi chake.Hakutaka tena
usumbufu wa kutoa mimba au kufikiria kondomu......
Tangu
wakati ule biashara yake iliimarika na wateja walizidi
kumiminika.Baada ya miaka kadhaa, Upako wa mwenyezi mungu
ulimfikia kupitia kwa mtumishi mmoja wa mungu ambaye alifanikiwa
kumfanya aokoke na kuwa mtumishi mzuri kanisani.....
Siku moja, mchungaji mmoja alimwita na
kumwambia kuwa:
"Dada yangu, Mwenyezi mungu amenena na mimi na kunifunulia
kuwa wewe ndo mke wangu wa ndoa, hivyo naomba tuoane.."
Mwanamke huyu alitabasamu na kusema:
"Kaka yangu, Mungu hajakwambia lolote, lasivyo, utakuwa
hujamsikia vizuri.Naomba uniache tu maana sina mpango wowote wa
kuolewa"
Yule mchungaji aliendelea kushikilia msimamo wake na kudai kuwa :
"Mungu amenifunulia,wewe ndo mke wangu"
Yule mchungaji aliendelea kushikilia msimamo wake na kudai kuwa :
"Mungu amenifunulia,wewe ndo mke wangu"
Mwanamke
huyu aliendelea kuyapuuza maneno hayo na ndipo sakata hilo lilipomfikia
Askofu wa kanisa hilo.....
Wakiwa mbele
ya mchungaji,Mwanamke huyu alifunguka kwa uwazi mbele ya askofu
na kudai kuwa kabla ya kuokoka
yeye alikuwa ni kahaba wa makahaba....
Askofu naye
alifunguka na kudai kuwa :"Sioni sababu
ya kuumiza kichwa kwa mambo yaliyopita.Mungu humsamehe mwanadamu
kwa kuzifuta dhambi zake zote za nyuma
na kumfanya awe mpya..!!!"
Mwanamke huyu alifunguka tena na kudai kuwa:
"Baba askofu, mimi nilishatoa kizazi changu
wakati nikiwa kahaba, kwa hiyo sitaweza kuzaa tena"
Askofu aliishiwa
pumzi baada ya kusikia hivyo.Hakuweza
tena kusema kuhusu kusahau ya nyuma.Ilibidi amgeukie yule mchungaji na kumwamba:
"Vipi, bado
kuna maono yoyote toka kwa mwenyezi mungu?"
Mchungaji
alijibu ,"Ndio,
huyu ndo mke wangu.."
Askofu ilibidi awaombee kwa sala maalumu.Hatimaye ndoa
ikafungwa......Baada ya miezi michache tu,
huyu mwanamke alibeba mimba.Yeye pamoja na mumewe waliongozana
pamoja kwenda hospitalini, tena kwa yule yule doctor aliyekitoa kile
kizazi......
Daktari
alipomuona alifurahi akidhani kuwa pengine mteja wake kamletea mteja mwingine.....Doctor hakuamini masikio yake baada ya kuambiwa kuwa huyu
mwanamke ni mjamzito na amekuja kujiandikisha clinic....
Hakika Mungu
ni Muweza wa yote....

Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment