Baadhi ya wasanii wakibadilishana mawazo kabla ya
mazishi.
Waombolezaji akina mama.
Dully Syaks (katikati) akiwa na mapacha Sunche na
Kapeto.
Baadhi ya wanamuziki wa kizazi kipya.
Mlevi nmmoja akicheza mbele ya waombolezaji.
Mwili wa marehemu ukisaliwa nyumbani kabla ya
kupelekwa makaburini.
Umati ukiwa tayari kwenda makaburini.
Vurugu zikiendelea wakati wa kwenda kuzika.
Vijana waliosababisha vurugu wakisukumana.
--------------------------------
MWANAMUZIKI mkongwe wa miondoko ya mnanda, Omar Omar Mfungilo,
ambaye alifariki usiku wa kuamkia ( Jumatatu) nyumbani kwao
Temeke-Mkoroshini amezikwa katika makaburi ya karibu na nyumbani
kwao.Mazishi hayo ambayo yalihudhuriwa na watu wengi, yalitawaliwa na vurugu ambazo zilisababisha baadhi ya waombolezaji kuporwa vitu vyao kama simu, pesa, saa na vitu vingine.
Wakati wa kwenda kumzika, vijana waliojiita ‘kikosi kazi cha mazishi’ waling’ang’ania jeneza lililobeba mwili wa marehemu na kulipeleka wao makaburini huku baadhi yao wakifanya vitendo vya uporaji njiani wakati wa kwenda kumzika.








Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment