Mkali wa mashairi na flow kutoka Mwanza
Fareed Kubanda a.k.a
Fid Q ametunukiwa cheti maalum cha shukurani na shirika linalosaidia
watu wenye
ulemavu wa ngozi(albino) linalojulikana ma Under The Same Sun kwa
mchango wake
mkubwa katika kusapoti kampeni ya shirika hilo.
Mwaka jana Fid Q akiwa na wasanii wengine wa
muziki wa
kizazi kipya na walizungukia mikoa ya kanda ya ziwa na kuwahamasisha
watu
kupinga mauaji ya albino wakiwa na shirika hilo.
baada ya miezi kadhaa walirudi tena kanda ya
ziwa
kuwarudishia shukurani wakaazi wa kanda ya ziwa kwa sababu mauaji ya
watu wenye
ulemavu wa ngozi (albino) yalipungua sana hivyo kampeni yao kwa
kushirikiana na
wakaazi wa kanda ya ziwa ilifanikiwa.

Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment