Imeandikwa na Samson
Chacha, HabariLeo, Tarime
SERIKALI imezuia kuingizwa nchini kwa mbegu za mahindi kutoka Kenya kutokana na kuibuka kwa ugonjwa wa mahindi ambao kitaalamu unaitwa Maize Lethal Necrotic Disease (MLND) nchini humo.
Habari zinasema kwamba ugonjwa huo umeonekana zaidi katika Bonde la Ufa, hususan eneo la Bomet, ambapo umeathiri zao hilo kwa kati ya asilimia 60 na 90 na umeelezwa kusambaa kwa kasi katika maeneo mengine ya Kenya.
Agizo la kuzuia mbegu za mahindi kutoka Kenya limetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Mohammed Muya kupitia barua yake ya Desemba 2012 iliyosambazwa katika vituo vyote vya Kilimo na Chakula katika Mipaka ya Tanzania na Kenya, kikiwemo Kituo cha Forodha ya Sirari.
Tayari utekelezaji wa agizo hilo umeanza ambapo shehena ya mbegu, zikiwemo za kampuni Kenya Seeds Maize imekamatwa na kuzuiwa katika eneo la Sirari.
Akizungumza na gazeti hili juzi ofisini kwake, Ofisa Kilimo na Chakula Kituo cha Sirari Mpakani, Phillipo Lusatola, alithibitisha kuzuiwa kwa mbegu hizo kutoka Kenya.
Huku akionesha shehena ya mbegu hizo, alisema: “Tumekamata mbegu hizo za mahindi kutokana na agizo la Serikali. Tutaendelea kukamata na kwa wakati huu tumeshabandika tangazo la karantini katika mbao za matangazo katika vituo vya mipakani zikiwemo ofisi za vijiji na kata kuwataarifu wananchi kuepuka kununua mbegu za mahindi kutoka Kenya kutokana na ugonjwa huo wa mahindi katika Bonde la Ufa.
“Tumefanya hivyo kwa sababu mbegu wakati mwingine husafirishwa na kuingizwa nchini kupitia njia za panya. Tunawatahadharisha wananchi kutonunua mbegu hizo hadi Serikali izifanyie uchunguzi wa kina katika kituo chetu kilichopo Arusha. Aidha, kwa wakati huu tunawashauri Watanzania kununua mbegu za Tanzania Official Seeds Cectutical ambazo zinapatikana hapa nchini na zimefanyiwa uhakiki kuwa ni salama kwa mkulima,” alisema.
Katika kituo hicho cha Kilimo Sirari, zimekamatwa katoni zaidi ya 10 za mbegu za mahindi zilizokuwa zinaingizwa nchini ambazo mara nyingi huuzwa kwa bei ya chini, hasa zinazopitishwa kinyemela kupitia vijiji jirani vya Kubiterere, Borega, Nyamohonda, Kogaja, Gosebe na Shirati na hatimaye kusafirishwa katika mikoa mingine nchini.

Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment