Chama kikuu cha Upinzani nchini
Ghana kimewasilisha kesi katika mahakama kuu zaidi nchini humo kupinga
ushindi wa rais John Mahama katika uchaguzi wa urais uliofanyika mapema
mwezi huu.
Chama cha National Patriotic Party (NPP)
kimepinga matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika tarehe Saba Desemba,
ikidai ulikumba na udanganyifu mkubwa.
Tume
ya uchaguzi nchini humo ilisema kuwa Bwana Mahakama alipata asilimia
50.7 ya kura zote zilizopigwa, idadi ambayo ni kubwa na hivyo kuepuka
duru ya pili ya uchaguzi dhidi ya mgombea wa chama cha NPP Nana
Akufo-Addo, ambaye alipata asilimia 47.7 ya kura.
Waangalizi wa kimataifa walisema uchaguzi huo
ulikuwa huru na wa haki.
Chama hicho cha NPP, kimesema imewasilisha kesi
hiyo baada ya kuchunguza takwimu kutoka kwa vituo elfu ishirini na sita
vya kupigia kura, vilivyokujwa na zaidi ya kura milioni kumi na moja.
Akufo-Addo alishindwa katika duru ya pili ya
uchaguzi wa urais mwaka wa 2008, kwa asilimia moja lakini alikubali
matokeo hayo.
Bwna Mahama wa chama cha National Democratic
Congress party, alikuwa makamu wa rais wa Ghana hadi kifo cha ghafla cha
rais wa hiyo hiyo John Atta Mills, mwezi Julai mwaka huu, ambako
aliteuliwa kuhudumu kama kaimu rais wa nchi hiyo.
Taifa la Ghana limekisiwa kuwa nchi iliyo na
demokrasia iliyokomaa na thabiti zaidi barani Afrika.
Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment