HABARI za tetesi zilizotapakaa katika mitaa ya jijini
hii leo ni kutokana na kutokomea kusikojulikana kwa mchezaji wa
kimataifa, Mrisho Ngassa, na kutojitokeza kwa ajili ya kufanya taratibu
za uhamisho wake wa kimataifa kwenda Sudan, ni kutokana na uamuzi
alionao mchezaji huyo wa kuamua kurejea katika Klabu yake ya zamani ya
Yanga.
Wakati muda uliotolewa na msemaji wa Klabu ya El
Merreikh ya Sudan, ukiwa unazidi kuisha kabla mchezaji huyo kujitokeza
na kumaliza taratibu za usajili huo wa kimataifa, imeelezwa kuwa hadi
sasa Ngasa bado hajapatikana na kwamba simu zake zote hazipatikani
hewani.
Chanzo cha habari hizi kilicho karibu na mchezaji
huyo na klabu ya Yanga, kimeeleza kuwa, Ngassa tayari amekubaliana
Klabu yake ya zamani ya Yanga na kwamba atajiunga na klabu hiyo baada
ya kumaliza mkataba wake wa mkopo wa miezi sita alioubakisha na klabu
ya Simba kwa malipo mazuri kama ambavyo imekuwa kwa mchezaji Haruna
Niyonzima.
"Ni kweli Ngassa tayari ameshakuwa na mazungumzo ya awali na Yanga
kwa miaka miwili, na tayari hivi sasa ameshapewa Sh. millioni 10 na
fedha nyingine atapewa mara atakapomaliza mkataba wake na Simba mwishoni
mwa msimu.
Sasa hivi Ngasa amejificha ili kuepeuka usumbufu wa
viongozi wa El Merreikh na Simba pamoja na Azam." kilisema chanzo hicho
Mrisho Ngassa amekuwa gumzo kubwa kwenye vyombo vya habari kuhusiana na
usajili wake kwa timu ya El Merreikh ambao walimuahidi mshahara wa
Dola 4000 kwa mwezi pamoja na Dola 75000 kama ada ya usajili, huku
vilabu vyake vya Simba na Azam FC vikilipwa Dola 100,000.
Kutokana na tukio hilo la kupotea kwa Ngasa, huku
timu ya El merreikh, ikimsubiri mchezaji huyo ili kujitokeza kwao na
kumaliza taratibu za usajili huo, tayari Uongozi wa Klabu hiyo umetoa
tamko .
Msemaji huyo wa El Merreikh,
Shekhe Idrissa, alesema kuwa tayari Klabu hiyo ilishafanya makubaliano
na vilabu vya Azam FC na Simba SC na mchezaji huyo na kilichokuwa
kimebaki ni kupatikana kwa mchezaji huyo na kutia saini mikataba pamoja
na kufanya vipimo vya afya ili mchezaji huyo aweze kujiunga na timu
hiyo tajiri ya Sudan, lakini muda mfupi baada ya kufika Dar es Salaam
mchezaji huyo amekuwa mafichoni - akiwa hapokei simu na muda mwingine
anazima bila kutoa taarifa zozote kwa vilabu husika.
"Mrisho Ngassa tulikuwa tumeshafanya nae mazungumzo vizuri na
tukakubaliana na ikabakia kumalizana na vilabu vya Simba na Azam, lakini
sasa tukiwa tayari tumemalizana na vilabu mchezaji mwenyewe amekuwa
akifanya vitendo visivyo vya kistaarabu, simu yangu hapokei na muda
mwingine anaizima kabisa''. alisema Shekhe
Hili sio jambo zuri kabisa kwake na kwa mpira wa
Tanzania kiujumla. Anaharibu sifa ya wachezaji wenzie wa kitanzania, ni
vizuri angepokea simu na kutueleza kama dili linawezekana au tofauti,
kuliko kutuacha sisi tukipoteza muda kuwepo hapa Tanzania huku tukiwa
njiapanda bila kujua kinachoendelea.
Kwa tabia hii ya Ngassa tumefikia
maamuzi ya kwamba mpaka kesho asubuhi (LEO) kama
hatapatikana, tutasitisha uhamisho wa mchezaji huyu na kuangalia sehemu
nyingine mbali na Tanzania." - Alimaliza Shekhe Idrissa.
Taarifa zilizoenea ni kwamba Ngassa hataki kwenda El Merreikh baada ya
kushawishiwa na viongozi wa Simba ili aendelee kuwepo Simba mpaka mkopo
wake utakapoisha mwakani na aweze kujiunga na klabu hiyo yake ya
zamani.
CHANZO: SUFIANI MAFOTO BLOG
CHANZO: SUFIANI MAFOTO BLOG

Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment