Hakuna tamu isiyokuwa nachungu! Kwenye ulimwengu wa mastaa Bongo
kulikuwa na matukio ya mengi ya kusikitisha mwaka huu lakini , Yafuatayo ndio mazito zaidi kwa mwaka 2012 SHEBBY D BLOG ina ripoti
kamili.
Matukio hayo ya huzuni yamegawanyika
makundi tofauti yakiwemo yale ya vifo, kuvunjika kwa ndoa na wengine
kutupwa rumande kwa misala mbalimbali.
Said
Fundi ‘Mzee Kipara’ na Steven Kanumba enzi za uhai wao
VIFO
Mwaka 2012 umepewa jina la mwaka wa shetani katika sanaa ya Kibongo
baada ya kufariki kwa vichwa kibao katika tasnia mbalimbali.
MZEE KIPARA
Mwanzoni mwa mwezi Januari,
mwigizaji wa siku nyingi Bongo, Said Fundi ‘Mzee Kipara’ alifariki dunia
akiwa kwenye nyumba ya Kundi la Sanaa la Kaole, Kigogo jijini Dar baada
ya kusumbuliwa na maradhi mbalimbali yaliyomuandama kwa muda mrefu na
utu uzima.
KANUMBA
Aprili 7, 2012, hali haikuwa shwari
katika tasnia ya filamu za Kibongo baada ya kufariki kwa ‘legendary’,
Steven Kanumba aliyepoteza uhai ghafla baada ya kudondoka nyumbani kwake
maeneo ya Hoteli ya Vatican, Sinza jijini Dar.
Mchezaji
wa Simba, Patrick Mafisango alivyo pata ajali na gari yake Toyota
Crestar Gx 100 hadi umauti wake ulipo mfika kwenye ajali hiyo
MAFISANGO
Mwezi Mei, mwaka huu, sekta ya michezo
nayo ilikumbwa na simanzi baada ya mchezaji wa Simba, Patrick Mafisango
kufariki dunia kwa ajali iliyotokea maeneo ya Tazara, Dar, wakati
akijaribu kumkwepa mwendesha bodaboda ambapo gari lake liliingia mtaroni
na hapo ndipo alipopoteza maisha.
MARIAM KHAMIS
Mwezi Novemba kilio
kilisikika kwenye muziki wa Taarab baada ya kufariki ghafla kwa staa wa
Kundi la Tanzania One Theater (TOT), Mariam Khamis ‘Paka Mapepe’
alipokuwa akijifungua.
MLOPELO
Pia Novemba mwaka huu, mwigizaji
aliyepata umaarufu mkubwa enzi za Kaole Sanaa Group kupitia runinga ya
ITV, Khalid Mohamed ‘Mlopelo’ alifariki dunia kwenye Hospitali ya
Temeke, Dar baada ya kuwa na maumivu ya mwili kwa muda mrefu.
JOHN MAGANGA
Kuonesha kuwa mwezi Novemba bundi
alikuwa ameng’ang’ania tasnia ya filamu za Kibongo, pia alifariki
mwigizaji John Stephano Maganga baada ya kuugua kwa muda mfupi na
kulazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar.
SHARO MILIONEA
Mwenzi huohuo wa
gundu, mwigizaji na mwanamuziki, Hussein Ramadhan Mkieti ‘Sharo
Milionea’, alifariki dunia kutokana na ajali ya gari iliyotokea usiku
katika eneo la Maguzoni Songa katikati ya Segera na Muheza mkoani Tanga
alipokuwa safarini kuelekea nyumbani kwao Muheza kumpelekea mama yake
fedha za matumizi.
LULU OSCAR
Pia ndani ya mwezi huohuo, aliyekuwa
Mtangazaji wa Kipindi cha Pepeta Afrika kunako SibukaTV, Dar, Lulu Oscar
alifariki ghafla akiwa nyumbani kwao Mbezi-Kwayusuf, Dar baada ya
kuzidiwa kwa kubanwa na kifua.
AMINA SINGO
Mwezi Desemba, fani ya utangazaji
nayo ilipata pigo baada ya kuondokewa na aliyekuwa Mtangazaji wa Kipindi
cha Afro-Vibes cha Times FM, Dar, Amina Singo aliyekuwa akiugua kwa
muda mrefu.
NDOA ZILIZOVUNJIKA
UWOYA
Ndoa ya staa wa filamu za Kibongo, Irene
Uwoya na mwanasoka wa Rwanda, Hamad Ndikumana ‘Kataut’ ilikuwa kwenye
msukosuko kwa muda mrefu lakini mwaka 2012 ndipo ule uzi uliokuwa
umeishikilia ulidaiwa kukatika.
JACK PATRICK
Modo wa Kibongo, Jacqueline Patrick
alifunga ndoa ya kifahari na mfanyabiashara Abdulatif Fundikira lakini
ndoa hiyo iliripotiwa kuota mbawa baada ya mumewe kutiwa mbaroni kwa
msala wa kusafirisha mihadarati ambaye anaendelea kusota nyuma ya nondo
za mahabusu katika Gereza la Keko, Dar.
DIDA
Mwaka 2012, mtangazaji mwenye jina kubwa
anayekitumikia kituo cha Radio Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida’,
alijikuta akirejea kwenye ukapera baada ya ndoa aliyofunga na mwanaume
aitwaye Gervas Mbwiga kuvunjika.
HUSNA MAULID
Mshiriki wa Miss Tanzania 2012,
Husna Maulid alifunga ndoa na jamaa aliyetajwa kwa jina moja la
Aboubakar ‘Abuu’. Hata hivyo, ndoa hiyo haikudumu kwani ilivunjika ndani
ya muda mfupi.
TITO
Ndoa ya mwigizaji wa filamu Bongo, Yusuf
Zimbwe ‘Tito’, aliyofunga na msichana wa mjini aitwaye Pamela Brown
iliota mbawa baada ya kutokea songombingo lenye ujazo mkubwa na
kusababisha wawili hao kufikishana mahakamani.
SKAINA
Staa wa filamu, Skyner Ally ‘Skaina’
ndiye ambaye ndoa yake na mwanaume aitwaye Saad Omary ilidumu kwa siku
chache kuliko nyingine kwani inakadiriwa kuwa na takriban siku nne huku
sababu ikielezwa ni kuolewa kwa staa huyo tayari akiwa na mimba ya
mwanaume mwingine.
NORA
Pia ndoa ya mwigizaji wa kitambo, Nuru
Nassor ‘Nora’ na Masoud Ally ‘Luqman’ nayo ilivunjika. Nora alidai kisa
cha ndoa kumshinda ni kutokana na mateso ya ajabu aliyokuwa akikutana
nayo hasa kutoka kwa ndugu wa upande wa mwanaume.
WALIOFIKISHWA POLISI
WEMA SEPETU
Katika kuandamwa na makasheshe,
mwaka 2012 haukupita hivihivi kwa Wema Sepetu kwani bidada alijikuta
akitupwa nyuma ya nondo Mabatini, Kijitonyama, Dar baada ya bangi
kukutwa nyumbani kwake. Hata hivyo, soo hilo lilimwangukia shosti wa
Wema aitwaye Jamilah Msafiri.
RICHIE
Kaka mkubwa kunako filamu za Kibongo,
Single Mtambalike ‘Richie’ alitiwa mbaroni kwa shitaka la kumshambulia
mpigapicha wa Kituo cha Runinga cha TBC1 aitwaye Moses.
AUNT EZEKIEL
Mwigizaji Aunt Ezekiel, hivi
karibuni alijikuta akisakwa na polisi baada ya kutuhumiwa kumpa kichapo
mrembo mmoja kisa kikielezwa kuwa ni mwanaume.
LULU
Mwaka 2012 hautasahaulika kwa Elizabeth
Michael ‘Lulu’. Bishosti alitiwa mbaroni na kusota mahakamani kwa msala
wa kuhusishwa na mauaji ya mwigizaji Steven Kanumba bila kukusudia.
KAJALA
Staa wa filamu Kajala Masanja alijikuta
mikononi mwa polisi hadi leo anasota mahabusu ya Gereza la Segerea, Dar
kwa msala wa kuuza nyumba iliyokuwa imewekwa kizuizini na Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), baada ya mumewe kufunguliwa
kesi ya kutakatisha fedha haramu.
LORD EYEZ
Rapa Waziri Makuto ‘Lord Eyez’ kutoka
Weusi alikamatwa na polisi baada ya kutuhumiwa kujihusisha na wizi wa
vifaa vya magari jijini Dar ambapo kesi yake inaendelea mahakamani.
JACK CHUZ
Mwigizaji Jacqueline Pentzel ‘Jack
Chuz’ alijikuta akitiwa mikononi mwa polisi katika Kituo cha Pangani,
Ilala baada ya kutuhumiwa kuchukua mshiko ili kuongoza filamu lakini
mwishoni aliingia mitini kwa madai kuwa aliokuwa akiwaongoza walikuwa
wakimdharau.
DIAMOND
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’
alijikuta matatani polisi baada ya kutuhumiwa kumshambulia mwandishi wa
Iringa, Francis Godwin ambapo kesi hiyo ilipofika mahakamani msanii huyo
alihukumiwa kifungo au kulipa faini.
SUMA LEE
Mzee wa Hakunaga, Ismail Sadick ‘Suma Lee’, naye mwaka 2012 alijikuta
akisakwa na polisi baada ya kutuhumiwa ‘kuchikichia’ mkwanja kwa ajili
ya shoo mkoani na kuingia mitini.
Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment