Gari aina ya Land Cruiser mali ya chuo cha SUA cha
mjini Morogoro kama linavyoonekana baada ya kupigwa mawe na watu
wanaodhaniwa kuwa ni majambazi nje kidogo ya mji wa Singida.
Mhudumu wa chumba cha kuhifadhia maiti cha
hospitali ya mkoa mjini Singida ambaye jina lake halikuweza kutambuliwa
mara moja, akiliweka sawa jeneza baada ya kufanyiwa ukarabati baada ya
kubomolewa na majambazi na kulisachi. (Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu.
Watu wasiofahamika idadi yao na ambao wanadhaniwa
kuwa ni majambazi, wamevamia gari lililokuwa linasafirisha maiti kutoka
Morogoro mjini hadi mkoa wa Mara na kupora zaidi ya shilingi milioni
19.8.
Baada ya kumaliza zoezi la uporaji huo, majambazi
hayo yalishusha jeneza na kisha kulifumua na kuanza kulisachi.
Jeneza hilo lilikuwa limebeba mwili wa mwanafunzi
Munchari Lyoba, mwanafunzi wa mwaka wa tatu aliyekuwa anasomea elimu ya
biashara kwenye chuo cha SUA.
Amesema gari hilo lilibeba viongozi wa wanafunzi
sita na viongozi wengine wanne akiwemo dereva.
Akizungumza na waandishi wa habari leo nje ya
chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya mkoa wa Singida, mkuu wa
msafara huo Makarang Nouna, amesema tukio hilo limetokea Disemba 6
mwaka huu saa 7.30 usiku, na lilihusisha gari Land Curise lenye namba za
usajili SU 37012 na lilikuwa likiendeshwa na Kalistus Malipula.
Amesema tukio hilo la kinyamana la kusikitisha,
limetokea katika barabara kuu ya Dodoma – Mwanza nje kidogo ya mji wa
Singida kwenye kona maarufu kwa jina la Mohammed Trans.
Amesema walipofika eneo la tukio, walikuta mawe
makubwa yamepangwa kukatisha barabara, kitendo kilichosababisha
washindwe kupita, na hivyo kutoa mwanya kuvamiwa na kundi kubwa la
vijana ambao walibeba bunduki mbili aina ya gobore, marungu, mashoka na
mawe.
Makaranga amesema walichofanya kwanza ni kupiga
kioo cha gari letu kwa mbele, na baadaye kumparaza kwa panga usoni
dereva wetu Kalistus Malipula.
Baada ya hapo walivunja vunja vyoo vyote na
kutuamuru kutoa kila kitu ambacho tulikuwa nacho.
Akifafanua zaidi, amesema kwa upande wake yeye
ameporwa shilingi milioni mbili ambazo zilikuwa kwa ajili ya kugharamia
msafara huo, jumla ya shilingi milioni 8.8 ambazo zilichangwa na
wanafunzi kama rambi rambi kwa mwenzao, na shilingi milioni tisa
ambazo wasindikizaji walikuwa nazo zikiwa ni posho.
“Pia tumeporwa simu zetu zote za mikononi, viatu,
laptop na mabegi yote ya nguo zetu”amesema.
Makaranga ambaye amesema anafanya kazi za kiutawala
katika chuo cha SUA, amewataja walioumizwa zaidi ni pamoja nay eye,
dereva Malipula na kiongozi wa wanafunzsi Idd Idd na kutibiwa katika
hospitali ya mkoa na kuruhusiwa.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Singida Mwalimu
Queen Mlozi, ambaye aliwasiliana na uongozi wa SUA Morogoro kwa ajili ya
shughuli ya kutuma gari jingine na ukarabati wa jeneza, amesema kuwa
kwa ushirikiano wa jeshi la polisi na kamati ya ulinzi na usalama,
watahakikisha watu waliofanya unyama huo, wanakamatwa mapema
iwezekanavyo ili waweze kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.
Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment