Skip to main content
HAYA NDO YALIYOMKUTA BAADA YA KUOMBA AGEUZWE KUWA MWANAMKE

Mwanamume
mmoja alimuomba Mungu amjalie ageuke kuwa mwanamke,kwa sababu alihisi
mke wake anafaidi kubaki nyumbani wakati yeye anapiga kazi masaa kumi
mfululizo.
Mungu hakuwa hiyana,asubuhi alipoamka,akajikuta
tayari amekuwa mwanamke.
Haraka haraka akamtayarishia 'mumewe'
chai,ili aende kazini,akaogesha watoto,akawapa chai na kuwatayarisha
kuwapeleka shule.
Wakati anarudi,akapitia sokoni kununua
mahitaji ya siku.Kufika nyumbani,akaanza kusafisha nyumba na kufua nguo.
Wakati anataka kutayarisha chakula,akagundua kuwa umeme umekatwa kwa
sababu ya deni,ikabidi atoke mbio kwenda kulipa bili ya stima.
Alipotoka kule,wakati wa kwenda kuwachukua watoto ulishafika,ikabidi
apitie shule. Kufika nyumbani,akaanza kutayarisha chakula huku watoto
wanamlilia njaa.
Kwa ufupi,hadi kufika wakati wa kulala,bado
hakuwa hajamaliza kazi zote,ikambidi aingie kitandani hivyo hivyo.
Kitadani nako hakukuwa na kupumzika.'Mume'alitaka
apewe kidogo,hakumkatalia.
Lakini baada ya kumaliza tu akamuomba Mungu: "Mungu
wangu,nimefanya
makosa,kwani kazi anazo fanya mke wangu ni kubwa kuliko nilivyokuwa
nikifikiria.Naomba unirejeshe katika hali yangu ya zamani."
"Hakuna taabu kiumbe wangu",Mungu
alimjibu na kuendelea,"Ombi lako
nimelikubali, lakini itabidi usubiri miezi tisa kwani jana ulipofanya
mapenzi na mume wako,ulishika ujauzito!!"
Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment