JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA
YA NISHATI NA MADINI
Mwezi Novemba 2012,
Kampuni ya Addax Energy SA ya Uswisi ilishinda zabuni ya sita ya
kuingiza mafuta kwa pamoja chini ya utaratibu unaosimamiwa na Kampuni ya
uagizaji mafuta kwa Pamoja (PICL). Zabuni hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya
mafuta ya Mwezi Desemba 2012 na mwanzoni wa Januari 2013.
Utaratibu wa uagizaji wa mafuta kwa pamoja huzingatia pamoja na mambo mengine viwango vya ubora wa mafuta kama vinavyoelekezwa na Shirika la Viwango nchini (TBS). Aidha, TBS hukagua ubora wa mafuta hayo kabla hayajaingia nchini.
Pamoja na aina nyingine za mafuta, Addax Energy SA ilipaswa kuleta mafuta ya dieseli yenye ujazo wa MT 100,000 sawa na takriban lita 100,000,000 katika zabuni ya sita. Meli ya AL BURAG iliyobeba mafuta hayo ilitakiwa kufika hapa nchini na kupakua mafuta kati ya tarehe 17 mpaka 20 Desemba 2012. Hata hivyo, meli hiyo ilifika tarehe 24 Desemba 2012 ikiwa imechelewa kwa siku nne kwa mujibu wa ratiba. Mafuta hayo yalipimwa na TBS tarehe 26 Desemba 2012 na kugundulika kuwa yako chini ya viwango vinavyotakiwa kwa Tanzania. Aidha, tarehe hiyo hiyo,
Kampuni binafsi ya Intertek Testing Services iliyoajiriwa na PICL pamoja na Addax Energy SA ilipima mafuta hayo na kujiridhisha kuwa yalikuwa chini ya viwango vinavyotakiwa.
Kwa kuzingatia hali hiyo Serikali imechukua hatua zifuatazo:
1. Imeiagiza PICL pamoja YARUDISHWE yalikotoka,
2. Imeiagiza EWURA ichukuwe hatua stahiki za KISHERIA dhidi ya Kampuni ya Addax Energy SA,
3. PICL ichukuwe hatua zinazotakiwa dhidi ya Kampuni ya Addax Energy SA kulingana na MKATABA, na
4. Imeziagiza PICL pamnoja na EWURA kuhakikisha kuwa hali hii haijirudii tena hapa nchini.
Aidha, Wizara ya Nishati na Madini inapenda kuwahakikishia wananchi kuwa kutopokelewa kwa mafuta hayo yaliyo chini ya viwango HAKUTAATHIRI upatikanaji wa mafuta ya dieseli nchini kwa kuwa kwa sasa kuna mafuta ya kutosha.
Katibu Mkuu
Dar es Salaam,
WIZARA
YA NISHATI NA MADINI
TAARIFA KWA
VYOMBO VYA HABARI
SERIKALI YAZUIA
KUINGIZWA MAFUTA YA DIESELI YALIYO CHINI YA KIWANGO NCHINI
Mwezi Novemba 2012,
Kampuni ya Addax Energy SA ya Uswisi ilishinda zabuni ya sita ya
kuingiza mafuta kwa pamoja chini ya utaratibu unaosimamiwa na Kampuni ya
uagizaji mafuta kwa Pamoja (PICL). Zabuni hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya
mafuta ya Mwezi Desemba 2012 na mwanzoni wa Januari 2013.Utaratibu wa uagizaji wa mafuta kwa pamoja huzingatia pamoja na mambo mengine viwango vya ubora wa mafuta kama vinavyoelekezwa na Shirika la Viwango nchini (TBS). Aidha, TBS hukagua ubora wa mafuta hayo kabla hayajaingia nchini.
Pamoja na aina nyingine za mafuta, Addax Energy SA ilipaswa kuleta mafuta ya dieseli yenye ujazo wa MT 100,000 sawa na takriban lita 100,000,000 katika zabuni ya sita. Meli ya AL BURAG iliyobeba mafuta hayo ilitakiwa kufika hapa nchini na kupakua mafuta kati ya tarehe 17 mpaka 20 Desemba 2012. Hata hivyo, meli hiyo ilifika tarehe 24 Desemba 2012 ikiwa imechelewa kwa siku nne kwa mujibu wa ratiba. Mafuta hayo yalipimwa na TBS tarehe 26 Desemba 2012 na kugundulika kuwa yako chini ya viwango vinavyotakiwa kwa Tanzania. Aidha, tarehe hiyo hiyo,
Kampuni binafsi ya Intertek Testing Services iliyoajiriwa na PICL pamoja na Addax Energy SA ilipima mafuta hayo na kujiridhisha kuwa yalikuwa chini ya viwango vinavyotakiwa.
Kwa kuzingatia hali hiyo Serikali imechukua hatua zifuatazo:
1. Imeiagiza PICL pamoja YARUDISHWE yalikotoka,
2. Imeiagiza EWURA ichukuwe hatua stahiki za KISHERIA dhidi ya Kampuni ya Addax Energy SA,
3. PICL ichukuwe hatua zinazotakiwa dhidi ya Kampuni ya Addax Energy SA kulingana na MKATABA, na
4. Imeziagiza PICL pamnoja na EWURA kuhakikisha kuwa hali hii haijirudii tena hapa nchini.
Aidha, Wizara ya Nishati na Madini inapenda kuwahakikishia wananchi kuwa kutopokelewa kwa mafuta hayo yaliyo chini ya viwango HAKUTAATHIRI upatikanaji wa mafuta ya dieseli nchini kwa kuwa kwa sasa kuna mafuta ya kutosha.
Katibu Mkuu
Dar es Salaam,
Comments
Post a Comment
toa maoni yako hapa pia usisahau kuweka coment