WALTER CHILAMBO NDIYE MSHINDI WA EBSS 2012


Mshindi wa shindano la  Epiq Bongo Star Search 2012 (EBSS),Walter Chilambo (Dar) akikabidhiwa sanduku lake lenye kitita cha shilingi milioni 50 usiku huu ndani ya ukumbi wa Diamond jubilee,katika shindano hilo lililovuta hisia za wengi,mshindi wa pili ameibuka mwanadada Salma Abushiri  (Zanzibar) na watu ni Wababa Mtuka (Dar)
Baadhi ya mashabiki wa mshindi wa shindano hilo la EBSS,Walter Chilambo wakishangilia kwa shangwe na vifijo mara baada kutamkwa yeye ndiye kinara katika kilele cha shindano hilo lililovuta hisia za watu wengi
Mkurugenzi wa kampuni ya Benchmark Productions Limited, na jaji mkuu wa Shindano la  Epiq Bongo Star Search 2012 (EBSS), akiwa amemkumbatia mshindi wa shindano hilo Walter Chilambo usiku huu ndani ya ukumbi wa Diamond,Chilamba ameibuka na kitita cha shilingi Milioni 50


WALTER CHILAMBO ndiye mshindi wa Shindano la Epic Bongo Star Search (EBSS)  2012. Kufuatia matokeo hayo Kalambo amejinyakulia kitita cha Shilingi Milioni 50 za Kitanzania kutoka kwa wadhamini wakuu wa shindano hilo kampuni ya Simu za Mkononi ya Zantel.
 Washiriki wa Washindano la EBSS 2012 ambao wamefanikiwa kuingia fainali ya shindano hilo wakiwa jukwaani usiku wa jana wakati wa kuanza kwa fainali hizo. Ni ndani ya Ukumbi wa Diamond Jijini Dar es Salaam. Mshindi kuondoka na kitita cha Shilingi Milioni 50 za kitanzania.

Comments